Ijumaa, 13 Oktoba 2017

MAHAKAMA YA TANZANIA YAKABIDHIWA LESENI YA UCHAPISHAJI WA JARIDA LAKE LA ‘HAKI BULLETIN’


Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania,  Mhe. Katarina Revokati (kulia) akikabidhiwa leseni ya uchapishaji wa Jarida la Mahakama kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi-Sehemu ya Usajili wa Magazeti, Idara ya HABARI-MAELEZO, Bw. Patrick Kipangula (wa pili kushoto), wanaoshuhudia zoezi hilo ni Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano-Mahakama ya Tanzania, Bw. Nurdin Ndimbe (wa pili kulia) na wa kwanza kushoto ni Bw. Samson Mashalla, Mtendaji wa Mahakama, anayeshughulikia Mahakama Kuu ambaye pia ni Mjumbe ya Bodi ya Wahariri (Editorial Board) ya Jarida la Mahakama lijulikanalo kwa jina la ‘HAKI BULLETIN’ linalotarajiwa kuanzishwa hivi karibuni.
Wakifurahia kwa pamoja mara baada ya kukabidhiwa leseni hiyo.
Msajili Mkuu (kulia) akionesha leseni hiyo kwa furaha mara baada ya kukabidhiwa tayari kwa kuanza rasmi uchapishwaji wa Jarida la Mahakama. Lengo la Jarida hilo litakalokuwa likiandaliwa na Kitengo cha Habari, Elim na Mawasiliano kwa ushirikiano na Bodi ya Uhariri-Mahakama ni kuuhabarisha Wananchi na Wadau wake juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea ndani ya Mahakama. Jarida hili litakuwa likipatikana pia 'online'
(Picha na Mary Gwera)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni