Jumatatu, 29 Januari 2018

KITUO CHA MAFUNZO NA HABARI KITAONGEZA UFANISI WA KAZI.



 Na Magreth  Kinabo 
JAJI Mkuu wa Tanzania  Profesa Ibrahim Juma   amesema  kwa  Kituo  cha  Mafunzo  na  Habari  cha Mahakama  kilichopo katika eneo la Kisutu jijini Dar es Salaam kitasaidia kuboresha  utendaji  kazi  kwa Watumishi  wa Mahakama na wadau wake.

Kauli hiyo ilitolewa na Jaji Mkuu Januari 29, 2018 wakati alipozindua  kituo hicho , ambapo  alisema  kitakuwa  ni sehemu ya  mafunzo  ya  kuweza kuendelea kuwajengea uwezo watumishi hao  na wadau Mahakama ili waweze kuwa na uelewa wa kutosha  wa masuala mbalimbali ya kisheria .

Aliongeza kwamba  kituo hicho, kielelezo cha Teknolojia  ya Habari  na Mawasiliano(TEHAMA)  hivyo  kinaweza kusaidia  watumishi  wa Mahakama  kutenda haki  kwa wakati, ikiwemo na kupata  habari.  
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Juma na Mkurugenzi  Mkazi  wa Benki ya Dunia(WB), Bellla Bird) wakikata  utepe  wakati  wakizindua  Kituo cha Mafunzo  na Habari  cha Mahakama kilichopo eneo la  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  jijini Dar es Salaam.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Juma na Mkurugenzi  Mkazi  wa Benki ya Dunia(WB), Bellla Bird  wakizindua   Kituo cha Mafunzo  na Habari  cha Mahakama kilichopo eneo la  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  jijini Dar es Salaam.
     Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Juma na Mkurugenzi  Mkazi  wa Benki ya Dunia(WB) wakiwasiliana  kwa njia video conference na baadhi  ya Watumishi  wa Mahakama na wanafunzi wadau walioko  Mnazimoja  kwenye Maonesho ya  Wiki  ya Sheria yanayoendelea hadi  Januari 31, mwaka  huu , wakati   wa kuzindua  Kituo cha Mafunzo  na Habari  cha Mahakama kilichopo eneo la  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  jijini Dar es Salaam.
 
 Jaji  Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Juma  akiwa katika picha ya Pamoja  na  baadhi  ya  viongozi  wengine wa Mahakama, watumishi , wakiwemo  wadau  wa mahakama.
Kituo  hiki kitasaidia  jiji la Dar es Salaam kuwa  na sehemu   ya mafunzo ya kisheria, kwa kuwa kitatoa mafunzo  ya kisheria  ili kuwajengea uwezo  watumishi  wa mahakama kuwa na uelewa  wa kutosha katika  masuala  ya Kielektroniki  na   kwenye  maeneo mapya ya kisheria ,” alisema Juma.


Baadhi ya majaji   wakiwa katika uzinduzi huo.
Profesa  Juma   alifafanua  maeneo hayo  kuwa  ni  makosa ya   kimtandao, makosa  yatokanayo na kuhamishwa  miamala  ya simu na dawa za kulevya, hivyo kinaweza kubaini kuwa mtu  akifanya kosa anaweza kufungwa  au kama ana hatia  kuachiwa.

Baadhi ya wageni  wakiwa katika uzinduzi huo.
(Picha na Lydia Churi)
 Aliwataka  watumiaji wa kituo hicho, kuhakikisha  kinakuwa na habari muhimu  kwa maendeleo  ya nchi ilinganishwa na nchi nyingine  ili kuifanya Tanzania  inakuwa  inafanya vizuri kuhusu  utekelezaji  wa mikataba na ubora wa ufanyaji biashara.

Kwa  upande wake, Mkurugenzi wa Mkazi kutoka Benki ya Dunia (WB) , Bellla  Bird alipongeza Mahakama ya Tanzania kwa juhudi zake  za kujenga kituo hicho  ambacho kinaongeza  ufanisi  wa utendaji  kazi  wa Mahakama  na  haki  inapatikana kwa wakati.

Naye Mkuu wa Chuo cha Uongozi  wa Mahakama(IJA), Mhe. Jaji  Paul  Kihwelo alisema kituo hicho kitakuwa  kinatoa  mafunzo  kwa njia vedio  kwa kushirikiano na IJA  na Mbeya .


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni