Jumapili, 28 Januari 2018

UZINDUZI WA WIKI YA SHERIA : JAJI MKUU AWATAKA WATUMISHI KUONGEZA IMANI YA MAHAKAMA

Na Lydia Churi-Mahakama

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka Watumishi wa Mahakama nchini kutoa huduma kwa kuzingatia Maadili, kuhakikisha kesi zinamalizika kwa wakati pamoja na kuacha vitendo vya rushwa ili kuongeza imani ya wananchi kwa Mhimili huo.

Akizindua wiki ya Sheria na Maonesho ya Elimu ya Sheria leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Jaji Mkuu alisema kuwa nguvu ya Mahakama ni imani ya wananchi na imani hiyo itaongezeka ikiwa hakuna rushwa, kuna maadili mema na kesi zitamalizika kwa wakati.

Jaji Mkuu pia amewataka wananchi kuacha kuilalamikia Mahakama na badala yake wachukue hatua kwa kuwataja watumishi wasiozingatia maadili kwa uongozi wa Mahakama.Aidha, amewashauri wananchi kujifunza na kuelewa taratibu za mashauri Mahakamani ili kurahisisha upatikanaji wa haki zao wanapozitafuta kwenye Mahakama mbalimbali nchini.

“Wananchi wengi wanakwenda kutafuta haki sehemu isiyohusika hivyo wanatakiwa kujifunza taratibu za Mahakama ili waweze kupata haki kwa wakati kwa kuwamuda mwingi unapotea  kwa  kutafuta haki mahali pasipostahili”, alisema Prof. Juma.

Alisema hivi sasa Mahakama inaingia kwenye matumizi ya Teknolojia ya habari na Mawasiliano- TEHAMA hivyo matumizi haya yatamsaidia mwananchi kuweza kufahamu hatua zote za shauri lake lililopo Mahakamani.

Jaji Mkuu ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Mnazi Mmoja ili kupata elimu juu ya masuala mbalimbali yanayohusu Mahakama na sekta ya sheria kwa ujumla.

Alisema, katika maonesho hayo, wananchi watapata nafasi ya kujifunza juu ya usuluhishi nje ya Mahakama,  Mahakama inayotembea (Mobile Courts) pamoja na changamoto  za upatikanaji wa haki zikiwemo upungufu wa Watumishi, Miundombinu, pamoja na vifaa.

Akizungumzia taratibu wa usuluhishi wa kesi nje ya Mahakama (Mediation), Jaji Mkuu amesema wakati sasa umefika kwa wananchi kutumia utaratibu huo unaorahisisha upatikanaji wa haki na kuongeza kuwa Haki bora hupatikana kwa usuluhishi majumbani.

Aidha, kabla ya kuzindua wiki ya Sheria, Jaji Mkuu aliongoza Matembezi waliyowashirikisha watumishi wa Mahakama, wadau pamoja na wananchi kwa ujumla yaliyoanzia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mpaka viwanja vya Mnazi Mmoja.


Matembezi hayo pia yalihudhuriwa na viongozi wa Serikali akiwemo Waziri wa wakati katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, Katibu Mkuu wa wizara hiyo  Prof. Sifuni Mchome pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju.


 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma wa pili kushoto akijiandaa kuanza matembezi rasmi kwa ajili ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria  leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam. Matembezi hayo yaliishia kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja. Wa kwanza kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi na wa kwanza kulia ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu na wa pili kulia ni Mke wa Jaji Mkuu mama Marina Juma.    
 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akijiandaa kuanza matembezi rasmi kwa ajili ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria  leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam. Wa pili kushoto ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali na wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome. Katikati ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglican nchini Tanzanaia.

 Bendi ya Polisi ikiongoza Maandamano hayo 

  Bendi ya Polisi ikiongoza Maandamano hayo 
  Bendi ya Polisi ikiongoza Maandamano hayo 


 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzanaia, Hussein Kattanga (wa pili kulia) wakati wa Matembezi ya Uzinduzi wa Wiki ya Sheria nchini leo jijini Dar es salaam.

 Jaji Viongozi wakipumzika baada ya kumaliza Matembezi 





 Mtendaji wa Mahakama Kuu, Leonard Magacha akifanya mazoezi baada ya kumaliza matembezi  


 Watumishi wa Mahakama pamoja na wadau wakisikiliza Hotuba ya Mgeni rasmi.
 Gari linaloonyesha mfano wa Mahakama inayotembea
 Jaji Mkuu wa Tanzania akioneshwa na Mkuu wa kitengo cha Maboresho ya Mahakama, Zahara Maruma namna  Mahakama inayotembea itakavyofanya kazi.
 Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revokati akioneshwa na Mkuu wa kitengo cha Maboresho ya Mahakama, Zahara Maruma namna  Mahakama inayotembea itakavyofanya kazi.

 Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali akizungumza
 Jaji Mkuu akizungumza





Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim (hayupo pichani ) pamoja na viongozi wengine wakiangalia na kushuhudia namna Video Conferencing inavyofanya kazi 
Mkuu wa kitengo cha Maboresho ya Huduma za Mahakama Mhe. Zahara Maruma akielezea kuhusu Maboresho ya Mahakama mbele ya Mhe. Jaji Mkuu pamoja na viongozi wengine.


(Picha na Lydia Churi na Mary Gwera)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni