Jumamosi, 27 Januari 2018

MAHAKAMA KIGOMA YAFANYA MATEMBEZI MAALUM KUASHIRIA UZINDUZI RASMI WA WIKI YA SHERIA NA SIKU SHERIA NCHINI, DC- BUHIGWE MGENI RASMI


Watumishi wa Mahakama za ngazi mbalimbali mkoani Kigoma wakiwa katika matembezi maalum kuashiria uzinduzi  rasmi ya Wiki ya Sheria, Matembezi hayo yameongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Kanali Maiko Gaguti (mwenye kapelo, aliyepo mbele) katikati ni Mhe. Flora Mtarania, Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma, mwenye tisheti nyeupe ni Kaimu Mtendaji Mahakama-Kigoma, Mhe. Humphrey Paya.

Baadhi ya Watumishi wa Mahakama-Kigoma pamoja na baadhi Wananchi wa Mkoa huo wakiwa katika matembezi, matembezi hayo yenye urefu wa umbali wa kilomita tatu (3) yalianzia katika eneo la Uwanja wa mpira wa Mwanga ‘Centre’ hadi Viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma 
Aidha Maonyesho ya Wiki ya Sheria Nchini yanafanyika katika Viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma, maonyesho haya yalioanza rasmi Januari 27 na kumalizika Januari 31, 2018 yanafanyika nchi nzima, kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini na Februari 01, 2018.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni