Jumamosi, 27 Januari 2018

MAONYESHO YA WIKI YA SHERIA YAANZA RASMI, WANANCHI WAFIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA KUPATA HUDUMA

Mkurugenzi wa Malalamiko na Maadili-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Happiness Ndesamburo akisikiliza malalamiko ya  mmoja wa wananchi aliyetembelea katika Banda hilo lililopo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Mahakama wakiendelea kuwasikiliza Wananchi waliotembelea katika Maonyesho hayo yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja na nchi nzima kuanzia Januari 27-Januari 31, 2018, kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini ni Februari 01, 2018 kitaifa itafanyika jijini Dar es Salaam na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa, Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, aidha sherehe hizi zinaadhimishwa nchi nzima.
2284: Muonekano wa Banda la Wizara ya Katiba na Sheria wakiwa katika Maonyesho ya Wiki ya Sheria nchini, yanayoendelea nchi nzima, Wizara ni Moja ya Taasisi za Sheria zinazoshiriki katika Maonyesho hayo, Taasisi nyingine ni: Tume Ya Utumishi Wa Mahakama, Ofisi Ya Mwanasheria Mkuu Wa Serikali (Agc), Ofisi Ya Mkurugenzi Wa Mashitaka (DPP ),  Mkemia Mkuu Wa Serikali, TAKUKURU (PCCB), Wakala Wa Usajili, Ufilisi Na Udhamini (Rita) na nyingine nyingi.
Muonekano wa sehemu ya Mabanda ya Watoa huduma ya Sheria pamoja na wananchi walipotembelea kupata huduma. limu ya Sheria ikiendelea kutolewa kwa wananchi walipotembelea Viwanjani hapo mapema Januari 27, 2018 siku ambayo Maonyesho yameanza rasmi. 
Elimu ya Sheria inaendelea nchi nzima,  pia kwa upande wa Dar es Salaam, huduma hii inatolewa katika Vituo mbalimbali kama Sinza (Simu 2000-Makmbusho), Magomeni (Manzese-Darajani), Mbezi Mwisho (ndani ya kituo), Kawe Stendi, Tegeta (Stendi Nyuki), Bunju, Mbagala Zakiem, Keko (Keko-Bora), Mjimwema-Kigamboni Stendi, Tandika mbele ya Kituo cha Polisi, Mombasa, Kitunda, Banana, Segerea, Ilala sokoni (Boma), Kariakoo-Msimbazi Polisi, Buguruni Sheli na Gerezani. (Picha na Mary Gwera)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni