JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA
UONGOZI WA MAHAKAMA YA
TANZANIA, UNAPENDA KUWATAARIFU NA KUWAALIKA WANANCHI WOTE KATIKA SIKU YA SHERIA
NCHINI INAYOASHIRIA KUANZA KWA MWAKA MPYA WA SHUGHULI ZA MAHAKAMA.
KATIKA KUADHIMISHA SIKU
HIYO, SIKU YA SHERIA NCHINI ITATANGULIWA NA WIKI YA UTOAJI WA ELIMU YA SHERIA
NA HUDUMA ZA MAHAKAMA KAMA SEHEMU YA MAADHIMISHO HAYO. UTOAJI WA ELIMU
UTAFANYIKA NCHI NZIMA NA KWA DAR ES SALAAM UTAFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA MNAZI
MMOJA KUANZIA TAREHE 27 JANUARI HADI TAREHE 31 JANUARI 2018 KUANZIA SAA 3:00
ASUBUHI MPAKA SAA 11:00 JIONI.
TAASISI ZITAKAZOKUWEPO NA
KUJUMUIKA NA MAHAKAMA YA TANZANIA KATIKA UTOAJI WA ELIMU NI PAMOJA NA:
·
TUME YA UTUMISHI
WA MAHAKAMA
·
OFISI YA
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI (AGC)
·
OFISI YA
MKURUGENZI WA MASHITAKA (DPP)
·
MKEMIA MKUU WA
SERIKALI
·
CHUO CHA UONGOZI
CHA MAHAKAMA (IJA)
·
MKUU WA KITIVO
CHA SHERIA, SHULE YA SHERIA UDSM
·
MKUU WA KITIVO
CHA SHERIA, CHUO KIKUU HURIA
·
TAASISI YA
MAFUNZO YA UANASHERIA KWA VITENDO TANZANIA (THE LAW SCHOOL OF TANZANIA)
·
TUME YA HAKI ZA
BINADAMU NA UTAWALA BORA
·
TUME YA
KUREKEBISHA SHERIA
·
TAASISI
ZINAZOTOA ELIMU NA MSAADA WA KISHERIA (LEGAL AID)
·
TAKUKURU (PCCB)
·
POLISI
·
MAGEREZA
·
MSAJILI,
MABARAZA YA ARDHI
·
CHAMA CHA MAWAKILI
TANGANYIKA (TLS)
·
TUME YA
KUREKEBISHA SHERIA
·
WAKALA WA
USAJILI, UFILISI NA UDHAMINI (RITA)
·
CHAMA CHA MAJAJI
WANAWAKE (TAWJA)
·
CHAMA CHA
WANASHERIA WANAWAKE (TAWLA)
·
SEKRETARIETI YA
MSAADA WA SHERIA
·
TUME YA
USULUHISHI NA UAMUZI (CMA)
·
LEGAL AND HUMAN RIGHT
CENTRE
·
BIMA YA AFYA YA
TAIFA
·
TPSF
·
TAMWA
KWA WALE WOTE WENYE MAHITAJI YA KUPATA MSAADA/ELIMU WA
KISHERIA, MALALAMIKO YOYOTE, MAONI AU MAPENDEKEZO YA UBORESHAJI WA UTENDAJI
KAZI WA MAHAKAMA WANAKARIBISHWA KUFIKA.
AIDHA YATAFANYIKA MATEMBEZI YA KUADHIMISHA SIKU YA
UTOAJI WA ELIMU YA SHERIA NCHINI. KWA DSM MATEMBEZI HAYO YATAFANYIKA SIKU YA
TAREHE 28JANUARI, 2018 SAA 12:00 ASUBUHI YATAKAYOANZIA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI
KISUTU NA KUISHIA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA. MATEMEZI HAYO YATAONGOZWA NA RAIS MSTAAFA WA AWAMU YA NNE
MHE.JAKAYA MRISHO KIKWETE
KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA
NCHINI KITAFANYIKA TAREHE 01.02.2018, KATIKA VIWANJA VYA MAHAKAMA VILIVYOPO
MTAA WA CHIMALA JIJINI DAR ES SALAAM. MGENI RASMI ATAKUWA RAIS WA JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI. SHEREHE HIZO
ZITAANZA RASMI SAA 03:00 ASUBUHI.
KAULIMBIU YA
MWAKA HUU: ‘’MATUMIZI YA TEHAMA KATIKA
UTOAJI HAKI KWA WAKATI NA KWA KUZINGATIA MAADILI’’
WOTE
MNAKARIBISHWA
IMETOLEWA NA:
OFISI YA MTENDAJI MKUU
MAHAKAMA
YA TANZANIA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni