JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAHAKAMA
TAARIFA KWA UMMA
RATIBA YA VIPINDI VYA
ELIMU YA SHERIA-WIKI YA SHERIA, 2018
NAPENDA
KUWAJULISHA KUWA TAREHE 26.01.2018 KATIKA KIPINDI CHA KIPIMA JOTO CHA ITV KUTAKUWA NA WAH. KUTOKA MAHAKAMA YA KAZI
WATAKAOSHIRIKI KATIKA KIPINDI HICHO KINACHORUSHWA KUANZIA SAA 03:00-5:00 USIKU
AIDHA
KUTAKUWA NA KIPINDI KINGINE TBC1 TAREHE 26.01.2018 SAA 01:00 USIKU
AMBAPO ATAKUWEPO MHE. WARSHA NG’HUMBU AKIZUNGUMZIA: MFUMO WA USHUGHULIKIAJI WA
MALALAMIKO NA MAADILI
JUMAMOSI,
JANUARI 27, 2018 KUTAKUWA NA KIPINDI KINGINE ‘POWER
BREAKFAST ON SATURDAY’ KINACHORUSHWA NA CLOUDS RADIO KUANZIA SAA 01:00
ASUBUHI KIKIZUNGUMZIA MFUMO WA USHUGHULIKIAJI WA MASHAURI YA ARDHI
JANUARI
29, 2018 KUANZIA SAA 12:00 ASUBUHI KUENDELEA
KUTAKUWA NA KIPINDI CHA MAHAKAMA: MSHIRIKI AMBAYE NI MKUU WA KITENGO CHA MABORESHO
‘HJDU’ MAHAKAMA YA TANZANIA ATAZUNGUMZIA MABORESHO YA MAHAKAMA.
JANUARI
30, 2018 KUANZIA SAA 12:00-01:00
ASUBUHI, MSAJILI-MAHAKAMA KUU YA TANZANIA, MHE. ILVIN MUGETA ATASHIRIKI KATIKA
KIPINDI CHA BARAGUMU KINACHORUSHWA NA ‘CHANNEL 10’ AKIZUNGUMZIA KUHUSU:
i.
HAKI NA WAJIBU WA MTEJA WA MAHAKAMA
ii.TARATIBU
ZA KUKATA RUFAA TOKA MAHAKAMA ZA MWANZO KWENDA MAHAKAMA YA WILAYA NA SHERIA
ZINAZOHUSIKA
FEBRUARI
01, 2018, TUTASHIRIKI KATIKA KIPINDI CHA MALUMBANO
YA HOJA KINACHORUSHWA NA ITV KUANZIA SAA 03:00-05:00 USIKU.
TUNATOA RAI MUWEZE KUANGALIA VIPINDI HIVYO NA KUWAJULISHA WENGINE KWA ILI
KUPATA ELIMU YA MAHAKAMA NA SHERIA KWA UJUMLA.
IMETOLEWA
NA: KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO
MAHAKAMA YA TANZANIA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni