Na
Mary Gwera
Jaji
Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka Majaji wapya wa
Mahakama Kuu ya Tanzania kufanya kazi kwa kiwango cha juu kwani wananchi wana
matarajio makubwa na matokeo ya kazi zao.
Alisema
hayo mapema Mei 07 alipokuwa akifungua Mafunzo Elekezi ya Waheshimiwa Majaji
wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania katika Kituo cha Mafunzo kilichopo katika
eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu-Dar es Salaam.
“Mafunzo haya yamekuja wakati
muafaka, wakati ambao Mahakama ya Tanzania ipo katika maboresho mbalimbali,
hivyo ni vyema ninyi Majaji kupitia utendaji kazi wenu mtumike kubadili taswira
ya Mahakama,” alisema Mhe. Jaji Mkuu.
Mhe. Jaji Mkuu alisema kuwa lengo
la Mafunzo hayo kwa Waheshimiwa Majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania ni
kuwapa miongozo na taratibu mbalimbali katika ufanyaji kazi ya Ujaji.
“Mafunzo haya endelevu
yanayotolewa na Mahakama kwa kushirikiana na Chuo cha Uongozi wa Mahakama
Lushoto ni muhimu katika utendaji kazi kwani baadhi ya Majaji walioteuliwa
wametoka sehemu mbalimbali hivyo ni vyema kuwafunza ili kuwa na uelewa wa
pamoja katika utendaji kazi,” alifafanua Mhe. Jaji Mkuu.
Mhe.
Jaji Mkuu pia amewataka Wahe. Majaji kufanya kazi kwa kuzingatia pia Dira ya Maendeleo
ya Taifa ya mwaka 2025.
Mafunzo
hayo yalioshirikisha jumla ya Majaji wapya 14, 12 kutoka Mahakama Kuu ya
Tanzania na wawili (2) kutoka Mahakama Kuu-Zanzibar yatafanyika kwa muda ya
Wiki tatu, na katika mafunzo hayo mada mbalimbali zitatolewa ikiwa ni pamoja na
Matumizi ya TEHAMA Mahakamani, Makosa ya Kimtandao nk.
Mafunzo
haya yanaendeshwa na Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Chuo cha Uongozi
wa Mahakama Lushoto chini ya ufadhili wa fedha za Mradi wa Benki ya Dunia.
Jaji Mkuu wa Tanzania ,
Mhe. Profesa Ibrahim Juma akifungua mafunzo elekezi ya wiki ya tatu kwa
ajili ya majaji wapya yaliyoanza leo kwenye Kituo
cha Mafunzo , kilichopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar e s Salaam.
|
Baadhi ya Majaji wapya wa Mahakama Kuu wakimsikiliza Jaji
Mkuu (hayupo pichani) wakati
ufunguzi wa mafunzo elekezi ya wiki
tatu yaliyoanza
leo kwenye Kituo
cha Mafunzo , kilichopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Majaji wapya wa Mahakama Kuu wa kimsikiliza (Jaji
Mkuu ,ambaye hayupo pichani wakati
ufunguzi wa mafunzo elekezi ya wiki
tatu yaliyoanza
leo kwenye Kituo
cha Mafunzo , kilichopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar e s Salaam.
|
Mkuu wa Chuo cha
Uongozi cha Mahakama(IJA) Mhe. Jaji Dkt .Paul Kihwelo akizungumza jambo katika mafunzo
elekezi wiki tatu kwa
ajili ya majaji wapya yayoanza leo
kwenye Kituo cha
Mafunzo , kilichopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar e s Salaam.
Majaji wapya wakiwa katika mafunzo elekezi ya wiki tatu yaliyoanza leo kwenye Kituo cha Mafunzo, Kilichopo Katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni