Jumanne, 12 Februari 2019

KESI PILI YA YASIKILIZWA KWA NJIA YA 'VIDEO CONFERENCE'



Na Magreth Kinabo
Mahakama ya  Kisutu leo imemsikiliza shahidi  aliyeko nchini China kwa njia mtandao  ‘video conferencing’ katika kesi ya uhujumu uchumi.

Kesi hiyo  namba  28 ya mwaka 2015 imesikilizwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi,Agustine Rwizile inamkabili raia wa Kichina Royce Lee ambaye anadaiwa kuwa na simu 30 na nyanya  ambazo zinawezesha kupiga simu nje ya nchi bila kulipa kodi kwa Mamlaka ya  Mawasiliano Tanzania  (TCRA.)

Katika kesi hiyo Shahidi Charles Okanda Nyatenga aliweza kutoa ushahidi wake kwa kutumia njia ya mtandao,ambapo alisema  anafahamu kuwa Royce ni rafiki na alimsadia kusajili  namba za simu kwa mitandao mitano
.
 Nyatenga alipoulizwa na Mwandesha Mashitaka Faraji Nguka  anafahamu vifaa vilivyokutwa  chumbani kwa Royce alikiri ana vifahamu.

 Kesi hiyo itasikilizwa tena Februari 25, mwaka huu
.
Hii ni mara ya pili kwa Mahakama hiyo kusikiliza kesi kwa njia ya mtandao na ni mara ya kwanza kusikiliza kesi ya jinai.

 Hakimu Mkazi Mwandamizi Agustine Rwizile (katikati kiti  cha mbele )akiendesha kesi ya jinai ya uhujumu uchumi kwa njia ya  mtandao ‘Video Conferencing’ katika Kituo cha Mafunzo kilichopo Kisutu jijini Dar es  Salaam.

Mwendesha Mashitaka  Faraja Nguka (katikati) akionesha vifaa vilivyo  kutwa  kwenye chumba cha Royce Lee,ambaye ni raia wa kichina.
   Wakili wa Royce Lee , Peter Kibatala akiwa katika kesi hiyo.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni