Jumanne, 3 Desemba 2019

JAJI MKUU AWAAPISHA MAHAKIMU WAKAZI NA KUKABIDHI NYENZO ZA KAZI


Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.Prof. Ibrahim Hamis Juma akimkabidhi nyenzo za kazi ‘instruments’ kwa Mhe. Godfrey Isaya za kuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Hakimu Mkazi-Kisutu. Hafla fupi ya kukabidhiwa nyenzo za kazi pamoja na kuapishwa Mahakimu Wakazi imefanyika katika Ukumbi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Arusha Desemba 03, 2019.
 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.Prof. Ibrahim Hamis Juma akimuapisha, Mhe. Upendo Moshi kuwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo, Mhe. Moshi ni mmoja wa Mahakimu wapya walioajiriwa hivi karibuni na Tume ya Utumishi wa Mahakama. 
 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.Prof. Ibrahim Hamis Juma akimuapisha, Mhe.          Veronica Mwanasenga kuwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo.
 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.Prof. Ibrahim Hamis Juma akimuapisha, Mhe. Oscar Kahyoza kuwa Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Serengeti.
 Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akimuapisha Mhe. Niku Mwakatobe kuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, kabla ya kuteuliwa kuwa Naibu Msajili, Mhe. Mwakatobe alikuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi-Arusha.

Pichani ni Naibu Msajili Mwandamizi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Messeka Chaba (aliyesimama), Mtendaji, Mahakama Kuu ya Tanzania, Bw. Leonard Magacha (aliyeketi- mwenye shati ya bluu bahari) na sehemu ya Watumishi wa Mahakama waliohudhuria katika hafla hiyo fupi ya Uapisho.
 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.Prof. Ibrahim Hamis Juma akizungumza na Wahe. Mahakimu aliowaapisha. Amewataka kuviishi viapo vyao na kujiepusha na vitendo vya rushwa na vilevile kutoa haki kwa wananchi kwa wakati na bila upendeleo.
 Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania pamoja na baadhi ya Majaji na Watendaji wa Mahakama wakiwa katika picha ya pamoja na Wahe. Walioapishwa na kukabidhiwa nyenzo za kazi.
 Picha ya pamoja na baadhi ya Majaji wa Mahakama ya Rufani walioshiriki katika hafla hiyo.

Picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji na Wasajili wa Mahakama.

(Picha na Mary Gwera, Mahakama-Arusha)








Hakuna maoni:

Chapisha Maoni