Jumatano, 4 Desemba 2019

MAFUNZO ELEKEZI KWA MAJAJI WAFAWIDHI YAENDELEA: MADA MBALIMBALI ZATOLEWA


MATUKIO KATIKA PICHA
Wahe. Majaji wakifuatilia mada inayotolewa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (hayupo pichani).
 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitoa Mada kwa Wahe. Majaji katika mafunzo elekezi yanayoendelea kutolewa kwa Wahe. Majaji Wafawidhi yanayofanyika katika Ukumbi wa ‘EAC’ jijini Arusha.
 Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Dar es Salaam, Mhe Rhoda Beatrice Mutungi akitoa mada inayohusiana na masuala ya Ukaguzi wa Mahakama kwa Wahe. Majaji Wafawidhi.
 Mkuu wa Kitengo cha Maboresho, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Zahra Maruma akitoa mada kwa Wahe. Majaji (hawapo pichani) juu ya Maendeleo ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa miaka mitano (5) wa Mahakama (2015/2016-2019/2020), Maeneo ya kuongeza nguvu pamoja na mipango ya baadae.
 Wahe. Majaji wakifuatilia mada inayotolewa.
 Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Divisheni ya Kazi, Mhe. Sophia Wambura akichangia jambo.
 Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Mbeya, Mhe. John Utamwa akichangia mada.
 Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu-Kanda ya Musoma, Mhe. John Kahyoza akichangia jambo katika mafunzo hayo.

Mmoja wa Wawezeshaji wa Mafunzo kutoka chuo cha ‘ESAMI’ Prof. Dkt. Michael Munkumba akitoa mada kwa Wahe. Majaji Wafawidhi.

Afisa Tehama, Mahakama ya Tanzania, Bw. Othman Kanyegezi akitoa mada kuhusu Mfumo wa kielektroniki wa Usimamizi wa Mashauri (JSDS II) unaotarajiwa kuwa chanzo rasmi taarifa zote za mashauri kuanzia Januari 01, 2020.
(Picha na Mary Gwera, Mahakama-Arusha)

 








Hakuna maoni:

Chapisha Maoni