Alhamisi, 20 Februari 2020

BENKI YA DUNIA YAISIFU KAMATI KUONDOA MBINU ZA KIUFUNDI



Na Magreth Kinabo - Mahakama

Jumla ya Sheria 38 zimefanyiwa uchambuzi, sheria 20 zimepitiwa na  Kamati ya Kanuni ya Jaji Mkuu, ambapo  sheria 9 zimekamilika   kwa ajili ya kuisaidia Mahakama ya Tanzania kuondoka na mbinu za kiufundi, ili kuiwezesha  kutoa haki na kumaliza mashauri kwa wakati.

Aidha  kanuni 41 zimepitiwa na kufanyiwa kazi ziko katika hatua za mwisho na kanuni 33 kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali kwa minajili ya kutumika. 

Akizungumza na wataalamu kutoka Benki ya Dunia,  (WB) leo  Mjumbe kutoka Sekretarieti ya  kamati hiyo, Mhe. Kifungu Mrisho, kutoka Kitengo cha Menejimenti ya Mshauri cha Mahakama ya Tanzania alisema  tayari utaratibu wa kuweka mabadiliko   ya Sheria 450 kupitia Mwanasheria Mkuu wa Serikali unaendelea.

‘‘Tumefanya maboresho ya sheria na kanuni ni kwa lengo la kurahisiha utaratibu mzima wa uendeshaji wa mashauri kuanzia hatua ya awali ya upokelewaji wa shauri hadi hatua ya mwisho kabisa ya utekelezaji wa tozo uliotokana na hukumu au uamuzi ama amri ya Mahakama, alisema  Mhe. Mrisho.

Kwa upande wake Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania,  kutoka Masjala Kuu ambaye ni Mjumbe wa kamati hiyo, Mhe.  Faiz  Twaib  alisema   ‘‘Tumefanya marekebisho makubwa  ya  sheria na kanuni mbalimbali, ambazo zimesaidia mashauri yaliyoko mahakamani kumalizika kwa wakati na tumepunguza mlundikano. Hivyo  kamati hii  ni moja ya kamati za Jaji Mkuu, ambayo iko hai na inatekeleza majukumu yake mara kwa mara,’’ alisema Mhe. Twaib.

Naye  Mtaalamu kutoka WB, Bw.  Waleed Malik aliipongeza Mahakama kwa hatua ya mabadiliko hayo.

 Mhe. alizitaja baadhi ya sheria zilizofanyiwa mabadiliko kuwa ni, Sheria ya Vyombo vya  Habari iliyotungwa mwaka 2017(Media Service Act of 2017), Sheria ya Migogoro ya Ardhi Sura Namba 216 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002 (Land Dispute Act Cap. 216 RE 2002) nayo imefanyiwa marekebisho na kuruhusu Wahe. Mahakimu wenye mamlaka ya nyongeza kusikiliza mashauri ya migogoro ya ardhi katika Mahakama Kuu ya Tanzania.

Nyingine Sheria za Madai na taratibu zake ya mwaka 2019, imepunguza hatua za usikilizwaji wa mashauri ya madai kutoka hatua 38 hadi hatua 22 tu zitakazo tumika mahakamani.

Mwaka 2016 kamati hiyo iliweza kupendekeza mabadiliko ya Sheria Sura Namba 141 ambayo ni Sheria ya Rufani inayotoa mamlaka ya kusajili rufaa katika Mahakama ya Rufani  ambayo haikuwa na kipengele cha mapitio.

Hakimu huyo aliongeza kwamba kamati hiyo,imefanya kazi zingine za kawaida za kuandaa maelekezo, miongozo na waraka mbalimbali.

Jaji wa  Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu, Mhe.Faiz  Twaib akizungumza jambo. akiwa katika  kikao cha  tathimini utendaji kazi zilizofanywa  na Kamati ya Kanuni  ya Jaji Mkuu, ukiwemo ujumbe wa Benki ya Dunia (WB). Kikao hicho kimefanyka leo kwenye ukumbi wa Maktaba  ya Mahakama ya Rufani  Tanzania , ambapo ujumbe  WB  umeipongeza  kamati hiyo kwa ufanisi wa maboresho ya sheria  na kanuni  ambazo zimesaidia  Mahakama kuondokana na mbinu za kiufundi  katika kutoa  haki kwa wananchi, ikiwemo kurahisisha umalizaji wa mashauri kwa wakati .

Wajumbe wakiwa katika  kikao cha  tathimini utendaji kazi zilizofanywa  na Kamati ya Kanuni  ya Jaji Mkuu, ukiwemo ujumbe wa Benki ya Dunia (WB). Kikao hicho kimefanyka leo kwenye ukumbi wa Maktaba  ya Mahakama ya Rufani  Tanzania , ambapo ujumbe wa   WB  umeipongeza  kamati hiyo kwa ufanisi wa maboresho ya sheria  na kanuni  ambazo zimesaidia  Mahakama kuondokana na mbinu za kiufundi  katika kutoa  haki kwa wananchi, ikiwemo kurahisisha umalizaji wa mashauri kwa wakati .

Ujumbe wa Benki ya Dunia  ukifuatilia tathimini hiyo.
Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia, Bw. Waleed Malik (katikati) akifafanua jambo leo katika kikao hicho,  wenzake (kushot)o ni   Bi. Debohar  Isser na Bi. Clara Maghani ( kulia).
Mjumbe wa Sekretarieti ya Kamati ya Kanuni, ambaye pia ni Hakimu Mkazi, Mhe. Kifungu Mrisho (kushoto wa kwanza), akiwasilisha leo tathimini ya utendaji kazi zilizofanywa  na Kamati ya Kanuni  ya Jaji Mkuu,  katika kikao hicho  kilichofanyika kwenye ukumbi wa Maktaba  ya Mahakama ya Rufani  Tanzania .
(Picha na Magreth Kinabo- Mahakama)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni