Jumatatu, 17 Februari 2020

JAJI MSTAAFU WA MAHAKAMA KUU MHE. KAZIMOTO AFARIKI


TANZIA
 Jaji Mstaafu Elias Kazimoto akiapishwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Rais wa awamu wa Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi Januari 6, mwaka 1986.
 
JAJI MSTAAFU WA MAHAKAMA KUU MHE. KAZIMOTO AFARIKI 

Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Elias Kazimoto amefariki Dunia leo mchana jijini Dar es salaam baada ya kuugua muda kwa muda mrefu.

Msiba wa Marehemu Jaji Kazimoto upo nyumbani kwake Kimara Korogwe jijini Dar es salaam na Tarehe ya Mazishi yatafanyika jijini Dar es salaam na tarehe itajulikana hapo baadaye.

Marehemu Jaji Elias Kazimoto alizaliwa Oktoba 9, mwaka 1942.

Aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Januari 6 mwaka 1985
Alistaafu kazi mwaka 1998 baada ya kuugua.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni