Ijumaa, 10 Julai 2020

PROF. MCHOME APONGEZA KASI YA MAENDELEO YA UJENZI WA JENGO LA IJC

Na Catherine Francis – Mahakama, Arusha
Katibu mkuu Wizara ya Sheria na Katiba, Prof. Sifuni Mchome amepongeza kasi ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) unaoendelea Jijini Arusha.

Pongezi zimetolewa na Mchome  alipotembelea na kufanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo,  Julai 9, mwaka huu, ambapo alisema kulingana na muda ambao  limeanza kujengwa hadi sasa hatua waliyofikia ni nzuri na inaridhisha.

‘‘Wahandisi wanaohusika na ujenzi huu endeleeni na kasi hiyo na ikiwezekana mmalize mapema zaidi kabla ya mwezi Desemba kama ilivyokubaliwa awali ili kuweza kuruhusu  upatikanaji wa huduma za kisheria kwa haraka na mapema zaidi,’’alisema  Katibu Mkuu huyo.

 Aidha Mchome  alipata nafasi ya kutembelea ofisi ya Jaji Mfawidhi  Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Mhe. Moses Mzuna ili  kuweza kujadili mafanikio na changamoto za ujenzi huo.

Naye Mtendaji Mahakama Kuu Kanda ya Arusha,  Bw.Edward Mbara, aliwasilisha  ripoti ya ujenzi huo na kuzitaja   changamoto kubwa  walizokumbana nazo kuwa  hali ya hewa ya mvua pamoja na ucheleweshaji wa malipo kwa wakandarasi kutoka  Hazina.

Akitatua changamoto ya uchelewashaji wa malipo hayo, alipiga simu kwa wahusika papohapo jambo ambalo lilipatiwa ufumbuzi  na kupewa majibu ya kuridhisha
Katika ziara hiyo Mchome  aliambatana na uongozi wa Mahakama Kuu  Tanzania Kanda ya Arusha walitembelea  ujenzi huo  ili kujionea hali halisi.


Katibu Mkuu wa  Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni  Mchome( kushoto)  akizungumza jambo  kwenye ofisi za eneo la ujenzi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) unaoendelea Jijini Arusha, kushoto ni  Jaji Mfawidhi  Mahakama Kuu  ya Tanzania Kanda ya Arusha Mhe. Moses Mzina.


Katibu Mkuu wa  Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome akiwa katika picha ya pamoja.


Katibu Mkuu wa  Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni  Mchome akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi za eneo la ujenzi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) unaoendelea Jijini Arusha, kushoto ni  Jaji Mfawidhi  Mahakama Kuu  ya Tanzania Kanda ya Arusha Mhe. Moses Mzina.
                                 (Na Catherine Francis – Mahakama, Arusha)


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni