Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 01 Oktoba, 2022 amewaapisha Mhe. Abubakar Amin Mrisha kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania pamoja na Mhe. Sylvester Joseph Kainda kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania. Uapisho huo ulijumuisha Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino jijini Dodoma.
Kuapishwa Mhe. Mrisha kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kunaifanya Mahakama Kuu ya Tanzania kuwa na idadi ya Majaji wapatao 99. Idadi hii ni kubwa kuwahi kutokea na inalenga kurahisisha jukumu la utoaji haki kikatiba kutekelewa kwa uwepesi na umahiri mkubwa.
Naye, Mhe. Kainda kabla ya
kuteuliwa na kuapishwa kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani alikuwa Naibu Msajili
wa Mahakama Kuu, Kanda ya Morogoro anachukua nafasi liyoachwa wazi na mtangulizi
wake Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Kevin Mhina.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Abubakar Amin
Mrisha (mwenye joho jekundu) kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino leo tarehe 01 Oktoba, 2022 jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Sylvester Joseph
Kainda (wa kwanza kulia) kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu
Chamwino mkoani Dodoma.
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi (mwenye joho jekundu) akiongoza Kiapo cha Maadili kwa Viongozi walioapishwa mara baada ya kuapishwa kwao na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwenye hafla iliyofanyika Ikulu
Chamwino mkoani Dodoma.
Viongozi walioapishwa wakiweka saini kwenye hati ya viapo vyao vya Maadili ya Viongozi wa Umma leo Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni