Na Fredrick Mahava-Mahakama, Sumbawanga
Baraza
la wafanyakazi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Sumbawanga lilikutana jana tarehe 15
Aprili 2024 katika ukumbi wa mikutano wa Mahakama kuu, Kanda ya Sumbawanga
kujadili masuala mbalimbali ya kiutumishi.
Akizungumza
wakati wa kufungua Baraza hilo, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga
Mhe.Dkt. Deo Nangela alisema utaratibu wa kuwa na mabaraza unalenga kukuza
uwazi na ushirikishwaji katika maamuzi mbalimbali ya utendaji kazi wa kila siku.
Mhe.
Dkt. Nangela alihimiza menejimenti ya Mahakama Kanda ya Sumbawanga na Chama cha
wafanyakazi (TUGHE) kushirikiana kwa
pamoja katika kutatua kero mbalimbali za watumishi ili kuongeza morali ya
watumishi hao ambao ni wachache na wanafanya kazi nyingi.
“Niwakumbushe
watumishi wenzangu kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na kujiepusha na vitendo
vya rushwa, pia mjikite katika shughuli mbalimbali za kujiongeza kipato kwani
mikoa hii ya Rukwa na Katavi ina fursa nyingi,” alishauri Mhe. Dkt. Nangela
Aidha,
wakati wa mkutano wa Baraza hilo kuliwasilishwa taarifa ya utekelezaji wa
shughuli za Mahakama Kanda ya Sumbawanga kwa kipindi cha kuanzia Julai 2023 hadi
Machi, 2024 ambayo iliwasilishwa na Kaimu Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya
Sumbawanga Bi. Irene Mlangwa
Vilevile,
Wajumbe wa Baraza hilo walijadili masuala mbalimbali ikiwemo mapitio ya Bajeti,
ukomo wa bajeti, utekelezaji wa bajeti, changamoto za utekelezaji wa bajeti, kupokea
na kujadili hoja za watumishi na pia majibu na ufafanuzi ulitolewa na viongozi
mbalimbali.
Wajumbe
waliohudhuria Baraza hilo kwa pamoja walikubaliana na kuweka mikakati ya pamoja
ya kutekeleza hoja mbalimbali ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi na pia
kuboresha baadhi ya mambo wakati wa Baraza lijalo.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Sumbawanga Mhe. Dkt. Deo Nangela (aliyenyoosha mkono) akiongoza Kikao cha Baraza la wafanyakazi Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga.
Katibu wa Baraza la wafanyakazi Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Bw.
Ayubu Nyallobi akisoma yatokanayo na Kikao kilichopita
Katibu wa TUGHE Mkoa wa Rukwa Bw. Amin
Msambwa (aliyesimama) akichangia hoja katika kikao cha Baraza hilo.
Mjumbe wa Baraza Bw. Jacob Mwakajengele
akichangia hoja wakati wa kikao hicho
Sehemu ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi
wakifuatilia hoja za kikao
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni