Jumatatu, 22 Aprili 2024

MAHAKAMA KANDA YA DAR ES SALAAM YAFANYA MAPINDUZI KATIKA UTENDAJI KAZI; JAJI MAGHIMBI

Na Eunice Lugiana, Mahakama-Pwani

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imefanya kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichoongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Jaji Mfawidhi wa Kanda hiyo, Mhe. Salma Maghimbi ambapo amesema kwa sasa Kanda hiyo amefanya mapinduzi katika utendaji kazi wake.

Akifungua kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti mwishoni mwa wiki iliyopita, Mhe. Maghimbi alisema kuwa, kwa miaka iliyopita Kanda ya Dar es Salaam imekuwa ya mwisho kwa utendaji kazi wake lakini kwa sasa imetoka kwenye kile Kituo ambacho ni cha mwisho kila mwaka lakini kwa sasa haiko hata kwenye wa pili kutoka mwisho.

“Naomba tujipongeze kwa hatua hii, nawashukuru pia watumishi wa ngazi zote maana kwa umoja wao wamechangia kufikisha Kituo mahali hapo maana hatupo mwisho wala kutoka mwisho hii ni juhudi katika kazi ndio imetufikisha hapa,” alisema Mhe. Maghimbi. 

Mhe. Maghimbi aliifananisha Kanda ya Da es Salaam na mtoto ambaye amekua mtukutu kwa kipindi cha nyuma lakini kwa sasa Kanda hiyo imeondoka huko kwa kasi na ndio maana inaonekana imefanya mapinduzi na sio mageuzi.

Aidha, Mhe. Maghimbi amewataka watumishi wa Mahakama Kanda hiyo kuwa na uadilifu upendo na ushirikiano maana muda mwingi unatumika wakiwa kazini.

“Nawakumbusha tu tunatumia muda mwingi sana kwenye sehemu zetu za kazi kuliko sehemu yoyote ya maisha yetu wengi tumeajiRiwa tukiwa na miaka 23 -24 unaenda kustaafu ukiwa na miaka 60 hivyo muda mwingi zaidi ya miaka 30 unautumia ukiwa kazini kwa hivyo huu ndio muda ambao tuko kwenye maisha yetu, tunaweza kufurahi tunajielewa tunaweza kufanya kitu chochote kwa hiyo tunatakiwa tuutumie vyema kuliko sehemu yoyote hii ndo sehemu ya kudumisha udugu kuongeza urafiki,” alisema Mhe. Maghimbi.

Kadhalika, Jaji Mfawidhi huyo aliwasihi watumishi wa Kanda hiyo, kuendelea kutumia TEHAMA kwakuwa kufikia Desemba Kanda ya Dar es Salaam huenda  majalada yote hayatakuwepo tena bali kila shauri litakuwa kwenye mfumo.

Vilevile, amewataka watumishi wa Kada zote kuijua mifumo yote ya Mahakama sambamba na kujiendeleza kielimu na sio kukaa na nafasi ambayo ameajiriwa nayo huku akitoa mfano kuwa, kuna Viongozi wa ngazi za juu za Mahakama wameanzia kwenye Kada za chini lakini leo hii ni Viongozi hii inafurahisha sana.

Awali, akimkaribisha Mhe. Jaji Maghimbi katika ofisi yake Mkuu wa wilaya ya Kibiti Mhe. Kanal Joseph Samwel Kolombo amemtoa wasiwasi Mhe. Jaji kwa kumuaminisha kua Kibiti iko salama hakuna matukio ya kiharifu yaliyopo ni ya kawaida tu ambayo wanaweza kukabiliana nayo.

Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Kanali Joseph Samwel Kolombo akizungumza na Jaji  Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Salma Maghimbi (hayupo katika picha) alipowasili Ofisi ya Wilaya ya Kibiti kwa ajili ya kikao hicho.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na waambata wake walipowasili Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kibaha kusaini kitabu cha wageni na kuzungumza na Mkuu wa Wilaya hiyo kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Kanda hiyo.

Katika picha ni Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Kanda hiyo, Mhe. Salma Maghimbi.


Meza Kuu ikiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, Mhe. Salma Maghimbi (katikati) Kutoka kushoto ni Katibu wa Baraza hilo, Mhe. Fahamu Kibona, Naibu Katibu, Lightness Kiula (Kulia), Mhe.Wilfred Dyansobera, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambaye ni Mgeni Mwalikwa katika kikao hicho na Mhe. Joyce Mkhoi, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Pwani Mwenyeji wa kikao hicho.


Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Sundi Fimbo (katikati) akiwasilisha taarifa ya mashauri katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi. Kushoto ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Livin Lyakinana na kulia ni Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Bw. Moses Mashaka.

 Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam wakifuatilia Kikao cha Baraza.

Meza kuu katika picha ya pamoja na Mahakimu Wafawidhi wa Kanda ya Dar es Salaam.

Maafisa Utumishi/Tawala, Afisa TEHAMA na Mkaguzi wa Kanda wakiwa katika picha ya pamoja na Meza Kuu.

Wawakilishi wa Chama cha Wafanyakazi (TUGHE) wakiwa katika picha pamoja na Meza Kuu.

Wasaidizi wa Majaji wakiwa katika picha na Meza Kuu.

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakifuatilia kikao cha Baraza kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti.

Meza kuu katika picha ya pamoja Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

(Habari hii imehaririwa na Mary Gwera, Mahakama-Dodoma)

 




 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni