Na Evelina Odemba – Mahakama, Morogoro
Menejimenti ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Morogoro, jana tarehe 15 Aprili, 2024 imefanya kikao kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji na uwajibikaji.
Kikao hicho, kilichoendeshwa na Mwenyekiti wake ambaye ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Morogoro, Mhe. Latifa Mansoor, kilipokea taarifa za Mahakama za Wilaya mkoani Morogoro ambapo wajumbe walipata wasaa wa kuweka mikakati mbalimbali.
Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Mansoor alisisitiza Mahakimu Wafawidhi wa Mahakama za Wilaya kuwa na utaratibu wa kupitia mara kwa mara Masjala za mashauri ili kujiridhisha na uhai wa taarifa zilizopo.
Sanjari na hayo, kikao hicho pia kilipokea taarifa za utekelezaji wa shughuli za kimahakama na kiutawala ambapo maazimio mbalimbali yaliwekwa ili kuhakikisha huduma ya haki kwa wananchi inawafikia kwa wakati.
Wajumbe walioshiriki kikao hicho ni Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Morogoro, Bw. Ahmed Ng’eni, Naibu Wasajili, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Mahakimu Wakazi Wafawidhi wa Mahakama za Wilaya na Maafisa Utumishi wao pamoja na wakuu wa vitengo ndani ya Kanda ya Morogoro.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Morogoro, Mhe. Latifa Mansoor akizungumza wakati wa kikao cha menejimenti.
Meza Kuu wakati wa kikao cha menejimenti ya Mahakama Kanda ya Morogoro. Kulia ni Jaji Mfawidhi, Mhe. Latifa Mansoor na kushoto ni Naibu Msajili, Mhe. Fadhili Mbelwa.
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Morogoro, Mhe. Susan Kihawa (kushoto) akiwa katika kikao hicho.
Sehemu ya wajumbe (juu na chini) wakifuatilia yaliyokuwa yanajiri wakati wa kikao.
Baadhi ya wajumbe (juu na picha mili chini) wakichangia hoja katika kikao hicho.
Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni