Na Lydia Churi- Tume ya Utumishi wa Mahakama- Ukerewe, Mwanza
Mkuu
wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Christopher Ngubyagai ameipongeza Tume ya Utumishi wa
Mahakama kwa mpango wake wa kutoa elimu kwa Wajumbe wa Kamati za Maadili ya
Maafisa Mahakama unaolenga kuwafikia wajumbe hao kwenye maeneo yao.
Akizungumza
jana wakati wa utoaji wa elimu kwa Kamati ya Maadili ya Maafisa Mahakama wilaya
ya Ukerewe, Mkuu huyo wa wilaya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili
ya Wilaya hiyo alisema njia iliyotumiwa na Tume kuwapatia elimu kwenye eneo lao
inasaidia kwa kiasi kikubwa kujenga uelewa mpana zaidi kwa wajumbe.
“Kwa
niaba ya Serikali ya wilaya ya Ukerewe, napenda kutoa pongezi za dhati kwa Mwenyekiti
wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma kwa kuwa na wazo la
kutoa elimu hii kwa wajumbe wa Kamati na pia kulitekeleza, tumejifunza mengi na
kupata uelewa mpana kuhusu Kanuni na Mwongozo wa Uendeshaji wa Kamati hizi”,
alisema.
Aidha,
Mkuu wa wilaya ya Ukerewe pia aliishukuru Sekretariet ya Tume ya Utumishi wa
Mahakama kwa kutekeleza uamuzi wa Tume wa kutembelea Mikoa na Wilaya kutoa
Elimu kuhusu utendaji kazi wa Kamati za Maadili kwa kuwafikia wajumbe wa Kamati
hizo moja kwa moja kwenye maeneo yao.
Katika
hatua nyingine, Mkuu huyo wa Wilaya ameipongeza Tume kwa kuanza kutekeleza
majukumu yake kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika Usaili
wa Watumishi wa Mahakama na pia kuandaa mfumo utakaorahisisha utendaji kazi wa
kamati za Maadili ya Maafisa Mahakama.
Akizungumzia
manufaa ya elimu waliyopatiwa, alisema yatawabadilisha wajumbe wa Kamati yake
na kuahidi kuwaelimisha wananchi kupitia mikutano ya hadhara ili nao waifahamu Tume
na kuitumia katika kutafuta haki zao.
“Wilaya
ya Ukerewe wananchi wake bado hawajafahamu zaidi uwepo wa Kamati ya Maadili ya Mahakimu
ya wilaya na jinsi gani wataleta malalamiko yao na changamoto wanazokutana nazo
kwenye Mahakama za Mwanzo ili waweze kupata haki”, alisema.
Alisema, akiwa Kiongozi na mlezi wa wilaya ya Ukerewe atafanya
kazi kwa ushirikiano wa karibu na wajumbe wa Kamati ya Maadili ya wilaya pamoja
na Mahakimu na kuwalea ili wananchi wapate haki na pia Serikali iliyoko
madarakani iendelee kukubalika na wananchi wake.
Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo cha kikatiba kilichopewa jukumu
la kusimamia uendeshaji wa Mahakama ya Tanzania. Moja ya jukumu lake ni kusimamia Maadili ya
Maafisa Mahakama ili kuhakikisha Mhimili wa Mahakama unatekeleza jukumu lake la
msingi na la kikatiba la kutoa haki kwa wananchi.
Jukumu la kusimamia Maadili ya Maafisa
Mahakama pamoja na majukumu mengine ya Tume, yameainishwa katika Ibara ya 11
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni