Jumanne, 21 Mei 2024

‘FUNGA MIRATHI UPATE HAKI YAKO KWA WAKATI’

Na. Tumaini Shita-Mahakama, Kinondoni

Wananchi wameombwa kufunga mirathi zao ili waweze kupata haki kwa wakati.

Kauli hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Kinondoni, Mhe. Olivia Towiro alipokua akitoa elimu kwa wananchi waliofika katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Kinondoni kupata huduma.

Zoezi la Utoaji huo wa elimu hiyo lilihudhuriwa na Mahakimu, watumishi wa kada mbalimbali na wadau.

Mhe. Towiro alielezea mambo mbalimbali kuhusu mirathi na umuhimu wa kufunga mirathi. Pia aligawa vipeperushi na formu za iirathi kwa wadau.

 Wakati wa zoezi hilo, wadau walipata nafasi ya kuuliza maswali ambayo yalijibiwa kwa ufasaha ili kuongeza uelewa kuhusu masuala ya mirathi kwa wananchi.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Kinondoni, Mhe. Olivia Towiro akizungumza alipokuwa akitoa elimu kwa wananchi waliofika katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Kinondoni.


Wananchi waliofika katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Kinondoni (juu na picha mili chini) wakishiriki zoezi la utoaji elimu.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni