Na Hilaly Lorry – Mahakama, Lindi
Mkandarasi kutoka kampuni ya Rizvi Engineering Ltd amekabidhiwa eneo kwa ajili ya kuanza ujenzi
wa Mradi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Mkoa wa Lindi.
Makabidhiano hayo yalifanyika hivi karibuni huku
yakushuhudiwa na Mkuu wa Kitengo cha Majengo cha Mahakama ya Tanzania Mhandisi Moses Lwiva na Mkandarasi Mshauri Mhandisi
Bw. Amri Mumba kutoka
kampuni ya Usanifu wa Majengo ya Y & P (T) Ltd na viongozi
mbalimbali wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi.
Mwenyekiti wa kikao hicho Bw. Amri Mumba alieleza kuwa ujenzi wa mradi wa Kituo Jumuishi cha
Utoaji Haki Lindi utachukua miezi tisa (9) hadi kukamilika na unatarajiwa
kuanza rasmi tarehe 09 Mei, 2024 na kukamilika 08 Februari 2025.
Aidha, Bw. Mumba alisisitiza mambo
mbalimbali ikiwemo jinsi ya kuratibu taka zinazozalishwa wakati wa zoezi la
ujenzi na kuwataka kutafuta namna bora yakuweza kuziharibu taka hizo ili
zisilete madhara kwa watu wanaozunguka eneo hilo la mradi.
Kwa upande wake, Mhandisi Moses Lwiva alimtaka Mkandarasi kujisajili kwa wakala wa usalama
na afya mahala pa kazi (OSHA).Vilevile kuzingatia sheria zote za usalama kwa
mafundi na watu watakao fika eneo la mradi kwani mradi huo ni wa Benki ya Dunia
huku akiwapa angalizo kuwa Benki ya Dunia wanazingatia usalama mahali pa kazi zaidi.
Mhandisi
Mshauri, Mkandarasi na timu nzima walikubaliana kufanya kazi kwa ushirikiano usiku na mchana kwa lengo la
kuhakikisha kuwa zoeli la ujenzi linakamilika kwa muda waliopewa ili kuwapunguzia gharama wananchi mkoani Lindi
kufuata huduma za kimahakama hasa
Mahakama kuu nje ya Mkoa wao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Mtendaji wa Mahakama
ya Hakimu Mkazi Lindi Bi.Quip Mbeyela
na Hakimu mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Mhe.Consolata Singano pamoja na
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Lindi Mhe. Maria Batulaine waliahidi kutoa
ushirikiano wa karibu na kufanya mawasiliano na pande zote zinahusika na ujenzi
huo kwa lengo la kuhakikisha ujenzi wa mradi huo unakamilika bila mkwamo wowote.
Makabidhiano ya mkataba kwa ajili ya ujenzi wa Kituo
Jumuishi cha Utoaji Haki Mkoa wa Lindi kati ya Mkandarasi kutoka Kampuni ya Rizvi
Engineering Ltd Bw.Ali Rivzi na Mkuu wa Kitengo cha
Majengo Mahakama ya Tanzania Mhandisi Moses
Lwiva kutoka Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania.
Mkandarasi kutoka kampuni ya Rizvi Engineering Ltd akionyeshwa eneo la ujenzi na mipaka yake.
Wajumbe wa
kikao cha makabadhiano wakifuatia kwa Makini wakati wa kikao.
Mtendji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Bi.Quip
Mbeyela (aliyevaa shati jeupe) wakitoa neno la ukaribisho wakati wa kikao cha
makabidhiano ya eneo la mradi wa ujenzi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Mkoa
wa Lindi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni