Alhamisi, 1 Agosti 2024

IMANI YA WANANCHI KWA MAHAKAMA KIGOMA YAPAA KWA ASILIMIA 50.78

Na Innocent Kansha- Mahakama, Kigoma

Elimu na uelewa wa wananchi dhidi ya shughuli za Mahakama za utoaji haki mkoani Kigoma vimezidi kuongeza imani ya wananchi kwa chombo hicho hili limethibishwa katika chati ya takwimu za wateja wanaofika Mahakama Kuu na Mahakama ya Hakimu Mkazi kupata huduma za kimahakama.

Ayo yalisemwa hivi karibuni na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Kigoma Mhe. Gadiel Mariki alipokuwa akifanya mazungumzo na Mkuu wa Kitengo cha Habari Mahakama ya Tanzania, Bw. Gerald Chami alipofika Mahakamani hapo kujitambulisha. Mhe. Mariki alisema, takwimu zinaonesha ongezeko kubwa la wananchi wanaofika mahakamani kupata huduma mbalimbali zinazotolewa.

“Mathalani ukiangalia takwimu za wananchi za mwezi Aprili hadi Juni, 2023 utaona jumla ya wananchi waliofika Mahakamani kupata huduma walikuwa 1,547 ukilinganisha na wateja waliopata huduma mahakamani katika kipindi cha mwezi Aprili mpaka Juni, 2024 idadi hiyo ilifikia jumla ya wananchi 3,143 ongezeko hilo ni sawa na asilimia 50.78 ya wananchi waliofika mahakamani kupata huduma mbalimbali za utoaji haki,” alisema Naibu Msajili huyo.

Mhe. Mariki alisema, wastani huo unadhihilisha wazi kuwa, wananchi wamejenga imani kubwa kwa chombo chao cha utoaji haki katika Kanda hiyo. Kwa kuendelea kutoa elimu kutasaidia kuimarisha imani ya wananchi kwa Mahakama, kukuza utawala wa sheria na kuondoa migogoro isiyokuwa ya lazima kwenye jamii.

Aidha, Mhe. Mariki alisema, utoaji wa elimu na kuimarisha imani ya wananchi kwa Mahakama kumechangia kiasi kikubwa kupunguza malalamiko katika kipindi cha robo mwaka ya April hadi Juni 2024, Jumla ya malalamiko yaliyobakia kipindi cha nyuma ni sefuri (0) yaliyopokelewa katika robo husika ni matano (5) na yote yaliyoshughulikiwa.

Elimu kwa umma, Mahakama Kanda ya Kigoma inao utaratibu wa kutoa elimu kwa umma kila Jumatano ya wiki kupitia Maafisa Mahakama wanatoa elimu hiyo kwa wananchi wanaofika Mahakamani kupata za huduma mbalimbali kwa siku hiyo. Aidha Kanda inautaratibu wa kutoa elimu kwa njia ya Redio ijulikanayo Joy FM inayorusha matangazo yake kutokea Kigoma mjini. Utaratibu huo ni wa siku mbili kwa mwezi yaani tarehe ya kwanza ya mwezi na tarehe ya mwisho ya mwezi.

“Hata hivyo, Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano cha Mahakama ya Tanzania kimeendelea na kuchukua taarifa za matukio mbalimbali ya shughuli za Mahakama na kuziweka katika mitandao mbalimbali ya kijamii ili kuongeza ufahama wa shughuli na matukio mbalimbali ya kimahakama,” alisema Naibu Msajili.

Kwa upande wa hali ya kuondoa mashauri mlundikano, Mhe. Mariki alisema, Mikakati mbalimbali imeendelea kuwekwa  kupitia vikao vya wadau ikiwa ni pamoja na vikao vya kususukuma mashauri (Case Flow Management na Bench Bar) ili  kuongeza ufanisi katika uondoshaji wa mashauri  kwa kuimarisha usimamizi bora wa mashauri kwa kuzingatia muda uliowekwa tangu kusajiliwa kwa shauri hadi kumalizika.

Aidha, katika kipindi cha April hadi Juni, 2024 Kanda ya Kigoma ilikuw ana mshauri 11 ya mlundikano kutoka Mahakama za Wilaya za Uvinza mashauri matatu (3), Kigoma mashauri saba (7) na Kakonko shauri moja (1).

Mahakama Mkoa wa Kigoma endelea kutoa mafunzo mbalimbali ya kuimarisha ufanisi na kuongeza weledi kwa watumishi kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Juni, 2024 jumla ya watumishi 95 kati ya watumishi 157 walipata mafunzo ya muda mfupi. 

Mafunzo hayo yalilenga maeneo tofauti tofauti kama vile mafunzo ya uendshaji mashauri ya mirathi, mafunzo ya mfumo wa kusimamia na kuratibu mashauri (e- CMS) mafunzo ya mfumo wa manunuzi (Nest) mafunzo ya kuanda matini ya kufundishia kwa njia ya masafa (e-Learning) na mafunzo ya Digital skills kwa Wasaidizi wa Kumbukumbu na Maafisa waendesha Ofisi. Hata hivyo watumishi 10 wapo kwenye masomo ya muda mrefu.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Kigoma Mhe. Augustine Karichuba Rwizile (aliyenyoosha mikono mbele) akifafanua jambo wakati alipotembelewa na  Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano cha Mahakama ya Tanzania, Bw. Gerald Chami (wa kwanza kulia) alipofika Ofisini kwake hapo kujitambulisha. Wengine ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Kigoma Mhe. Gadiel Mariki (wa kwanza kushoto) na Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Kigoma Bw. Filbert Matotay (wapili kushoto).

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Kigoma Mhe. John Francis Nkwabi (aliyeketi mbele) akiteta jambo wakati alipotembelewa na  Mkuu wa Kitengo cha Habari Elimu na Mawasiliano cha Mahakama ya Tanzania, Bw. Gerald Chami (wa kwanza kushoto) alipofika Ofisini kwake hapo kujitambulisha. Wengine ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Kigoma Mhe. Gadiel Mariki (wa kwanza kulia)

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Kigoma Mhe. Projestus Kahyoza (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano cha Mahakama ya Tanzania, Bw. Gerald Chami (wa kwanza kulia) wakati alipomtembele kumsalimia wakati wa ziara ya kujitambulisha Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma. 

Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano cha Mahakama ya Tanzania, Bw. Gerald Chami (wa kwanza kulia) akifanya mazungumzo na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Kigoma Mhe. Gadiel Mariki (wa kwanza kushoto) mbele ni Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Kigoma Bw. Filbert Matotay.

Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Kigoma Bw. Filbert Matotay akiteta jambo na Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano cha Mahakama ya Tanzania, Bw. Gerald Chami (wa kwanza kushoto) na kulia ni Afisa Utumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Kigoma Bw. Festo Sanga

(Picha na Innocent Kansha- Mahakama)











 

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni