Jumamosi, 7 Septemba 2024

JAJI MKUU AWASILI RWANDA KUHUDHURIA MKUTANO WA KIMATAIFA KUHUSU HAKI MAZINGIRA

Na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Kigali

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma leo tarehe 7 Septemba, 2024 amewasili nchini Rwanda kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Chama cha Majaji na Mahakimu kutoka Jumuiya ya Madola.

Mhe. Prof. Juma na ujumbe wake amewasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Kigali majira ya saa 12.10 jioni na kupokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Mhe. Maj. Gen. Ramson Godwin Mwaisaka na Mwambata Siasa, Mhe. Moses E. Moses.

Katika Mkutano huo wa siku tano, Jaji Mkuu ameongozana na Majaji wawili wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Barke Sehel, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) na Mhe. Dkt. Paul Kihwelo.

Wengine ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani na Majaji wengine wa Mahakama Kuu, Mhe. John Kahyoza, ambaye pia ni Rais wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT), Mhe. Ilvin Mugeta, Mhe. Butamo Philip, Mhe. Yohana Massara na Mhe. Dkt. Adam Mambi.

Viongozi wengine ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Nkya, Msajili wa Mahakama ya Rufani, Mhe. George Herbert, Katibu wa Jaji Mkuu, Mhe. Venance Mlingi, Katibu wa Jaji Kiongozi, Mhe. Aidan Mwilapwa na Katibu wa Msajili Mkuu, Mhe. Dkt. Jovin Bishanga.

Wapo pia Viongozi wa JMAT, Mhe. Shaibu Mzandah, Mhe. Lazaro Magai, Mhe. Nemes Mombury, Mhe. Adeline Kashura, Mhe. Mary Kallomo na Mhe. Devota Ksebele na Mhe. Hassan Chuka ambaye pia ni Katibu wa Msajili wa Mahakama ya Rufani.

Watumishi wengine wa Mahakama walioambatana na Jaji Mkuu ni Bw. Fadhili Mgutta na Bw. Juma Mshana.

Ujumbe huo wa Mahakama ya Tanzania unahudhuria Mkutano huo utakaofanyika kuanzia kesho tarehe 8 Septemba, 2024 katika Ukumbi wa Kimataifa Kigali.

Mkutano huo wenye kauli mbiu ya “Haki Mazingira” umeandaliwa na Jumuiya ya Madola kwa kushirikiana na Mahakama ya Rwanda.

Katika Mkutano huo, Majaji na Mahakimu watajadili vipengele mbalimbali vya kisheria na kitaasisi ili kuimarisha usimamizi na upatikanaji wa haki kuhusiana na mazingira na jukumu kuu la Mahakama katika kudumisha haki mazingira. 

Kupitia mada na mijadala mbalimbali, wajumbe wa Mkutano huo watakuwa na fursa za kubadilishana uzoefu kati yao na kuunda uhusiano wa kudumu miongoni mwao.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (kulia)  akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Mhe. Maj. Gen. Ramson Godwin Mwaisaka baada ya kuwasili jijini Kigali, Rwanda kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Chama cha Majaji na Mahakimu kutoka Jumuiya ya Madola. 

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akielekea kwenye mapumziko. Picha chini ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani.


Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, ambaye pia ni Rais wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT), Mhe. John Kahyoza akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kigali pamoja na Viongozi wengine wa Mahakama. Anayeangalia kamera ni Katibu wa Jaji Kiongozi, Mhe. Aidan Mwilapwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni