Na Evelina Odemba – Mahakama Morogoro
Kocha Mkuu wa Mahakama Sports, Spear Mbwembwe ametoa tahadhari kwa timu zote zinazotegemea kushuka dimbani dhidi ya Mahakama kwa kuwa Mahakama imejipanga zaidi kutoa kichapo kikali bila huruma.
Mbwembwe ametoa kauli hiyo mara baada ya Mahakama kuibuka kidedea kwa siku mbili mfululizo katika michezo yote iliyoshiriki katika mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) inayoendelea mjini Morogoro.
Kocha huyo alisema kuwa siri kubwa ya mafanikio imepatikana baada ya kuwa Timu hizo zimepata muda mzuri wa kukaa kambini, zimezingatia maelekezo waliyopewa na inatarajia ushindi kila ilatapopata nafasi ya kushuka dimbani na timu yeyeote itakayokuja mbele yake.
“Kiukweli kama kocha nina furaha sana, kuanzia jana na leo Mahakama inarudisha shukurani kwa mashabiki kwa kuhakikisha inaibuka kidedea, hatuna hofu kwa timu yeyote ile tutakayocheza nayo iwe upande wa kamba, mpira wa miguu au mpira wa pete sisi ni kushinda tuu, nina uhakika kwani nawaamini sana wachezaji wangu” alihitimisha Kocha Mbwembwe kwa furaha.
Maelezo hayo ya Kocha Mbwembwe yanapewa uzito na matokeo mujarabu ya timu za Mahakama dhidi ya wahasimu wao na kupitia matokeo hayo washindani wanaitafsiri kuwa ni onyo kwao.
Katika Michezo mbalimbali ambayo mahakama imeshiriki imehakikisha inaibuka kidedea katika michezo yote huku hatua hii ikitafsiriwa kuwa ni onyo kali linalotolewa na mahakama dhidi ya timu yeyote itakayoshuka nayo dimbani.
Akielezea matokeo upande wa Mahakama katika mashindano hayo yanayoendelea Mjini hapa Mwenyekiti wa Mahakama Sports Willson Dede alisema kuwa mpaka sasa mahakama haijapoteza katika mchezo wake wowote .
Akifafanua kwa upande wa mchezo wa kamba wanamme (ME) waliwanyanyasa Kamba (ME) toka Maadili huku Kamba wanawake (KE) ikiwavuta bila huruma katiba na sheria katika mchezo wao wa tarehe 20 Septemba, 2024 wakati huo huo leo tarehe 21 Septemba, 2024 Kamba Me toka Mahakama ikiibuka mshindi dhidi ya Afya Ke. Wakati huo huo Kamba Ke Ikijitwalia ubingwa dhidi ya timu toka Haki.
Upande wa mpira wa miguu bado Mahakama imeendelea kuwa tishio baada ya kuibuka washindi katika mechi mbili tofauti walizocheza ambazo ni Mahakama kuibamiza timu ya Wizara ya Utamaduni mabao Matano (5) kwa sifuri (0) hapo jana tarehe 20 Septemba, 2024 ushindi huo umeendelea hadi hivi leo tarehe 21, septemba, 2024 ambapo Mahakama ikijipatia gori moja kwa sifuri dhidi ta timu toka ofisi ya Waziri Mkuu Sera.
Aidha nako upande wa Mpira wa Pete jana tarehe 20 Septemba, 2024 Mahakama iliitandika bila huruma mabao 42 kwa 19 waliyoambulia timu ya Maadili, wakati leo tarehe 21 Septemba, 2024 Mahakama imeibuka mshindi wa mabao 35 kwa 25 waliyoambulia mambo ya nje.
Michezo ya SHIMIWI inategemea kufunguliwa rasmi hapo tarehe 25 Septemba, 2025 na kuhitimishwa tarehe 5 Octoba, 2024.
Kikosi cha mpira wa miguu toka Mahakama Sports Club kikiwa uwanjani.
Matukio katika picha wakati timu ya Mpira wa Miguu toka Mahakama ikichuana na timu toka Waziri Mkuu, Sera.
Matukio katika picha wakati timu ya Mpira wa Pete toka Mahakama ikichuana na timu toka Mambo ya Nje.
(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dar es Salaam)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni