Ijumaa, 13 Septemba 2024

TANZIA; HAKIMU MKAZI MFAWIDHI MASASI AFARIKI DUNIA

Marehemu Batista Kindaga Kashusha enzi za uhai wake.

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake Mhe. Batista Kindaga Kashusha aliyekuwa akihudumu Mahakama ya Wilaya Masasi mkoani Mtwara kwa Cheo cha Hakimu Mkazi Mfawidhi.

Kwa mujibu wa Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mtwara, Bw. Yusuph Msawanga, marehemu Batista amekutwa na umauti alfajiri ya leo tarehe 13 Sept, 2024 alipokuwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Masasi - Mkomaindo.

Taarifa zaidi kuhusu msiba huu zitatolewa baada ya mipango ya mazishi kukamilika.

Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha kuomboleza msiba wa mpendwa wetu.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni