Ijumaa, 31 Januari 2025

ELIMU YA SHERIA MTAANI MATAWI YA JUU USIPIME YAWA MWAROBAINI KWA WANANCHI

Na INNOCENT KANSHA – Mahakama, Dodoma

Maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini yamezidi kushika kasi wakati zoezi la kutoa elimu ya sheria kwa wananchi katika viunga vya jiji la Dodoma likipata mwitikio mkubwa, huku elimu iliyoonekana kuwavutia wanananchi wengi wa viunga hivyo ikiwa ni ya Mirathi, Ndoa, Talaka, Madai, Utekelezaji wa hukumu, Utatuzi wa migogoro ya Ardhi, Usalama wa Raia na Mali zake na Elimu ya Usalama Barabarani, dhahiri ikionesha kuwa ni mwarobaini wa matatizo ya kisheria kwa wananchi.

Akizungumza na wananchi kwa nyakati tofauti katika Soko la Maisha Plus (Bonanza) Chamwino na Stendi ya mabasi ya Chamwino Makore jijini Dodoma leo tarehe 31 Januari, 2025 Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Hawa Mguruta akitoa darasa la Ndoa na Talaka amesema, kuna aina kuu tatu za ndoa mosi ndoa ya mke mmoja, ndoa ya wake wengi na ndoa inayothaniwa kuwa ya wake wengi.

“Kuna imani zimejengeka miongoni mwa jamii zetu zinazosema eti kwamba, ukikaa na binti wa mtu kwa muda wa miezi sita tu, eti huyo anaaminika kuwa mke wako halali kisheria si kweli. Ukweli ni kwamba, kisheria ili mke na mume watambulike kama mke na mume kuna kitu kinaitwa dhana ya ndoa. Dhana hii kisheria inasema ni lazima wawili hao waishi pamoja kwa muda wa zaidi ya miaka miwili wakishudiwa na majirani na jamii inayowazunguka wakiishi paa moja, wakiishi hivyo, kisheria watatambulika na itahesabika kama mke na mume ama ndoa halali kwa jicho la kisheria,” amesisitiza Mhe. Mguruta.

Aidha, Mhe. Mguruta amebainisha kwamba, kuna aina tatu ya ndoa ila kuna aina tatu ya namna ndoa zinavyofungwa na kusherehekewa katika jamii, moja ni kwa njia ya Kimila, kwa njia ya Kikristo na kwa njia ya Kiislamu. Aidha ndugu wananchi hizi siyo aina za ndoa bali ninamna ndoa zinavyofungu kulingana na imani na tamaduni za jamii husika.

Akitoa elimu kuhusu ufunguaji wa mashauri ya ndoa mahakamani, Naibu Msajili hiyo amesema, ili ufungue shauri la ndoa kuna vitu viwili vya muhimu unapaswa kuzingatia cha kwanza lazima ndoa inayotakiwa kuivunja iwe na umri wa zaidi ya miaka miwili. Hivyo mtu yeyote ambaye ndoa yake haijafikisha miaka miwili hawezi kufungua shauri la ndoa mahakamani.

“Ispokuwa kama kutakuwa na sababu za msingi za kupewa ruhusa na Mahakama kwa maana ya kwamba ukitaka kufungua shauri la ndoa kabla ya kutimiza miaka miwili ni sharti uende mahakamani na uiombe Mahakama ikupe ruhusa ya kufungua shauri hilo, na sababu pekee ni kwamba, kuna mazingira fulani fulani magumu yasiyoweza kuvumilika katika hali ya kawaida. Endapo Mahakama ikiridhika sababu za mleta maombi itatoa ruhusa ya kufungua shauri hilo la ndoa,” ameongeza Mhe. Mguruta.

Jambo la pili la msingi ili mtu aweze kufungua shauri la talaka ni lazima ndoa hiyo iwe imesuluhishwa na Baraza la Usuhishi la Kata au Uongozi wa Kanisa au Baraza la Kiislam Bakwata kulingana na imani ya mtu anayetaka kufungua shauri la talaka kwa ajili ya usuluhishi. Na endapo vyombo hivyo vitashindwa kuwapatanisha watatoa fomu namba tatu (3) ambayo muhusika ataitumia kwenda mahakamani kufungua shauri la ndoa. “Sasa ukipata fomu namba tatu utaiambatanisha fomu hiyo kwenda nayo mahakamani na utaomba kufungua shauri lako,” ameongeza Naibu Msajili huyo.

Mhe. Mguruta amesema, shauri hilo la ndoa unaweza kulifungua Mahakama ya Mwanzo, Mahakama ya Wilaya, Mahakama ya Hakimu Mkazi ama Mahakama Kuu. Mahakama zote hizo zina mamalaka zinazofanana.

“Endapo unataka kufungua shauri hilo, ila hujui udai vitu gani, kwenye shauri la ndoa unaweza kuomba nafuu zifuatazo kwanza kabisa unaweza kuomba talaka, kwamba ndoa yako ivunjwe na upewe talaka kuonyesha usitisho wa ndoa yako, lakini pia unaweza kuomba uangalizi wa watoto, kwa maana ya nani anastahili kuishi na watoto kati ya wanadoa waliotalakiana. Lakini pia unaweza kuomba matunzo ya watoto na upande uliotalakiwa ambao Mahakama itatoa matunzo hayo kwa kuzingatia maslahi mapana ya watoto. Vilevile anaweza kuomba amri ya watoto wasisumbuliwe na wenza uliyetalakiana,” amesisitiza Mhe. Mguruta.

Vilevile, akifafanua hatua za rufaa kwenye mashauri ya ndoa ama talaka, Mhe. Naibu Msajili amesema, ikiwa hujaridhika na amri ama hukumu iliyotolewa unapaswa ufanye nini? Sheria inakuruhusu ukate rufaa. Kama shauri la talaka lilisikilizwa Mahakama ya Mwanzo utakata rufaa kwenda Mahakama ya Wilaya na kama lilikuwa linasikilizwa Mahakama ya Wilaya au Mahakama ya Hakimu Mkazi utakata rufaa kwenda Mahakama ya Kuu na pia kama shauri lilisikilizwa na Mahakama Kuu utakata rufaa kwenda Mahakama ya Rufani ya Tanzania.

“Na rufaa hizi kutoka Mahakama yoyote niliyoitaja hapo juu inatakiwa maombi hayo ya rufaa yaombwe ndani ya siku arobaini na tano (45) na mtu akizidisha siku hizi bila kukata rufaa ni lazima kwanza kabla ya kukata rufaa yake apeleke kwanza maombi ya nyongeza ya muda wa kukata rufaa akieleza sababu za kumsababisha kutokufanya hivyo ndani ya muda uliotajwa kisheria,” amefafanua.

Kwa upande wake, mdau wa Mahakama ya Tanzania kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka nchini, Mwendesha Mashtaka Mwandamizi Bw. Hebel Kihaka akitoa elimu kwa wananchi amesema, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ilianzishwa kama Ofisi huru ya umma kupitia Tangazo la Serikali namba 49 la Mwaka 2018 la tarehe 13 Februari,2018 la kuanzishwa kwa Mamlaka hiyo kwa ajili ya kutekeleza mamlaka ya kikatiba aliyopewa Mkurugenzi wa Mashtaka ya kusimamia haki jinai kwa mujibu wa Ibara ya 59B ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

“Wajibu wa Msingi ni kushirikiana na wadau ikiwepo Mahakama kuendesha kesi za jinai bila woga, upendeleo au ubaguzi ili kuhakikisha haki, amani na usalama vinatamalaki katika jamii,” amesema Mwendesha Mashtaka huyo.

Majukumu ya Msingi ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ni kusimamia uendeshaji wa mashauri ya jinai kote nchini, kusimamia na kuratibu shughuli za upelelezi, uchnguzi wa mashauri yote ya jinai, kutoa ushauri wa kisheria kwa mamlaka mbalimbali katika masuala ya kijinai, kuendesha na kusimamia mashauri ya utaifishwaji wa mali zinazohusianav na uhalifu.

Vilevile, kuratibu mashauri yanayohusiana na uhamishwaji wa wahalifu kutoka ndani na nje ya nchi katika masuala ya jinai.

Wakati zoezi la kutoa elimu ya sheria kwa wananchi katika viunga vya jiji la Dodoma likipata mwitikio mkubwa, mtaani kwetu kulikuwa na kazi, shwangwe na nderemo.

Wakati zoezi la kutoa elimu ya sheria kwa wananchi katika viunga vya jiji la Dodoma, Dogo Janja hakubaki nyuma akitokomea na machapisho ya mashauri ya watoto kusambaza upendo

Kaka Mkubwa umakini mkubwa akichuja elimu ya sheria kupitia kipeperushi maadhimisho wiki ya sheria mtaani jiini Dodoma.

Wakati zoezi la kutoa elimu ya sheria kwa wananchi katika viunga vya jiji la Dodoma washikaji wa Bodaboda hawakubaki nyuma kupata elimu hiyo

Wakati zoezi la kutoa elimu ya sheria kwa wananchi katika viunga vya jiji la Dodoma washikaji wa Bodaboda hawakubaki nyuma kupata elimu hiyo.

Wakati zoezi la kutoa elimu ya sheria kwa wananchi katika viunga vya jiji la Dodoma washikaji wa Bodaboda hawakubaki nyuma kupata elimu hiyo.


Wakati zoezi la kutoa elimu ya sheria kwa wananchi katika viunga vya jiji la Dodoma washikaji wa Bodaboda hawakubaki nyuma kupata elimu hiyo.




Kaka Mkubwa hakubaki nyuma katika kujielimisha namna ya kuzifikia huduma za Mahakama ya Tanzania wakati wa zoezi la kutoa elimu ya sheria kwa wananchi katika viunga vya jiji la Dodoma.





Wakati zoezi la kutoa elimu ya sheria kwa wananchi katika viunga vya jiji la Dodoma hakuna ambaye hakufikiwa hata kwa wa mama wachuuzi wa samaki walifikiwa 


Wakati zoezi la kutoa elimu ya sheria kwa wananchi katika viunga vya jiji la Dodoma Koplo Ester Makali akitoa ufafanuzi wa masuala ya Jeshi la Polisi.

Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Hawa Mguruta akitema madini ya mirathi kwa wananchi huku akimkonga mwoyo.










Wakati zoezi la kutoa elimu ya sheria kwa wananchi katika viunga vya jiji la Dodoma Koplo Ester Makali akitoa ufafanuzi wa masuala ya Jeshi la Polisi.















(Picha na Innocent Kansha - Mahakama)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni