. Mhe. Jaji Nongwa atema cheche Sheria Rushwa ya Ngono Chuo Kikuu Mzumbe Mbeya
. Usafirishaji haramu wa binadamu elimu yatolewa juu ya sheria ya uhamiaji
DANIEL SICHULA- Mahakama, Mbeya
Timu ya elimu kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya, pamoja na wadau wengine wa sheria wametembelea Taasisi mbalimbali za Serikali katika jiji la Mbeya, ikiwepo Chuo Kikuu Cha Sayansi na Teknolijia Mbeya (MUST), Chuo Kikuu cha Mzumbe Mbeya, Shule ya Msingi Azimio, Shule ya Msingi Sisimba, Shule ya Sekondari Sangu na Ivumwe Sekondari.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya,Mhe. Joachim Tiganga alitoa elimu ya Mihimili ya Dola namna inavyofanya kazi kwa wakufunzi na wanachuo wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) katika ukumbi wa mikutano wa chuo hicho kwenye ukumbi wa Nyerere.
Elimu ya mirathi iliyotolewa katika chuo hicho iliibua maswali mengi kutokana na washirki wengi kutokuwa na uelewa juu ya sheria ya mirathi na ndoa.Baada ya elimu kutolewa na timu ya Mhe. Jaji ilijenga uelewa mpana kwa washiriki na kupelekea baadhi ya washiriki kutaka kujua ni namna gani ya kuandika wosia kabla ya mtu kufariki, namna ya kutunza wosia.
Aidha katika Chuo Kikuu cha Mzumbe Mbeya, Mhe Jaji Victoria Nongwa na timu yake kutoka Mahakama Kuu Mbeya pamoja na wadau wengine washeria akiwepo Wakili kutoka Ofisi ya Mashtaka ya Wakili Mkuu wa Serikali Mbeya, walitoa elimu juu ya rushwa ya ngono na rushwa kiujumla katika maeneo ya kazi kwenye Taasisi za Serikali na zisiszo za Serikali.
Wakati huo huo timu nyingine ya watoa elimu walifanikiwa kupita na kutoa elimu katika shule kadhaa za sekondari na msingi za Mkoani Mbeya na mada mbalimbali zinazohusu haki ya watoto na wajibu wa mzazi na mlezi katika makuzi ya watoto,ukatili wa kijinsia na namna bora ya kuishi na watoto.
Pia ilitolewa elimu juu ya sheria za uhamiaji ambapo waligusia suala la usafirishaji wa binadamu ikizingatiwa Mbeya ni moja ya Mikoa inayopakana na nchi jirani za Malawi na Zambia. Na timu hii iliongozwa na Hakimu Mfawidhi Mahakama Mkoa Mbeya Mhe. Zawadi Laizer.
Mhe. Tiganga alipowasili katika chuo cha MUST alipokelewa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma na Ushauri wa Kitaaluma Prof. Said Vuai akiwa pamoja na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango,Fedha na Utawala Prof. Zacharia Katambara alipowasili katika viua alitoa elimu ya Mihimili ya Dola namna inavyofanya kazi kwa wakufunzi nga vya Chuo Kikuu cha MUST Mhe. Tiganga alipata wasaa wa kuzungumza mwandishi wa habari wa Radio ya MUST FM, ambapo alisema
“Katika kuadhimisha wiki hii ya sheria, Mahakama na wadau wote wa sheria wapo katika maeneo mbalimbali ya jiji la Mbeya na Viunga vyake kutoa elimu mbalimbali juu ya masuala yanahusu sheria, hivyo basi wakati huu ni fursa kwa wananchi kupita maeneo hayo kujifunza na kupata msaada juu ya mambo kadha wa kadha yanayohitaji kutatuliwa kisheria,”.
Timu ya watoa elimu MUST wakiwa kwenye picha ya pamoja na Uongozi wa MUST.
Washiriki.
(Habari hii imehaririwa na Magreth Kinabo- Mahakama, Dodoma)


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni