Na Magreth Kinabo- Mahakama, Dodoma
Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Winfrida Beatrice Korosso, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria, Mhe.Winfrida Beatrice Korosso amesema kitendo cha Mahakama ya Tanzania kushiriki wadau Mahakama wa na taasisi zingine katika Maonesho ya Wiki ya Sheria kimesaidia kuwarahisishia wananchi kupata elimu ya sheria kwa upana na nyinginezo.
Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 29 Januari, 2025 na Mhe. Korosso mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea Kitaifa katika Viwanja vya Nyerere ‘Square, jijini Dodoma.
“Washiriki wa ari ya kuelimisha umma masuala ya kisheria na ukatili wa kijinsia na kumsikiliza mwananchi, hivyo kitendo cha wadau na taasisi ambazo ni washirika na Mahakama na mjumuiko wa taasisi zisizo wadau wa Mahakama kushiriki katika maonesho haya kimesaidia wananchi kupata elimu ya sheria kwa upana sambamba na elimu nyingine,” amesema Mhe.Jaji Korosso.
Jaji Korosso amesema kuwa anatoa shukrani kwa Uongozi wa Mahakama ya Tanzania kwa kutoa elimu ya sheria na masuala haki, hivyo maonesho hayo ni muhimu kwa wananchi kwa kuwa hata baadhi ya taasisi zingine zimeshiriki. Huku akisisitiza kwamba maonesho hayo yana mabadiliko chanya kwani yametimiza malengo yake ya kuhakikisha haki inatendeka,pia yamemrahisishia mwananchi kufikiwa na vyombo vya sheria vinavyoweza kumsaidia huku akiongeza kwamba amefurahi kukutana na taasisi zingine.
Akizungumza kuhusu Tume anayeiongoza amesema ina uhuru wa kuishauri Serikali kubadilisha sheria ili ziende na wakati. Hata hivyo ameongoza kuwa sheria zinaishi na zinatakiwa ziendane na matakwa ya jamii.
“Tume hii imekuwa ikifanya utafiti wa masuala ya kisheria,kuna umuhimu wa kushirikisha sekta nyingine kama vile udaktari au mtaalaum wa dawa ili kupanua wigo kuwa na wajumbe kutoka fani ya udaktari, ili kuboresha utafiti wetu,” amesisitiza Mwenyekiti huyo.
Aidha Jaji huyo amefafanua kuhusu suala la Haki Madai ambapo amelizungumzia kuwa ni eneo ambalo lina athari kwa mwanachi bila kujua na lina uhusisha mahusiano ya kila siku mfano mahusiano ya ndoa,biashara ujasiamali hivyo ili kuweza kuendane na Dira ya Taifa ya Maendeleo ni lazima wajikite na kuweka msingi ambao mwananchi aweze kuelewa mfano eneo la mirathi.
Jaji huyo pia alitembelea Banda la Tume ya Utumishi wa Mahakama, Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanznia(TAWJA), Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.
Wakati huohuo,Mwakilishi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Bw.Ipiana Murilo, ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa Divisheni ya Utaratibu na Huduma za Ushauri wa Kisheria alitembelea banda la Mwanasheria huyo na kupewa maelezo kutoka kwa Wakili wa Serikali Mwandamizi kuwa ofisi hiyo imeanzisha kamati za kudumu za Ushauri za Mikoa na Wilaya na wanavyoendelea kufanya kiliniki za bure za sheria mikoani.
Pia alipata maelezo kutoka banda la Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevyia kuhusu dawa za kulevya na dawa za binadamu zinaweza kuleta madhara ya uraibu. Dawa hizo ni Mophine, Tramadol, Phenobabitone, Ketamine, Skanka na Valium. Pia alipewa maelezo kuhusu namna ya kupata kibali cha kusafiri kwa njia ya elektroniki kutoka Idara ya Uhamiaji, likiwemo suala madhara ya uhamiaji haramu.
Banda lingine alilolitembelea ni Mahakama ya Afrika Mashariki, Mamlaka ya Rufani za Dhabuni za Umma, Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF), Idara ya Kazi na Wakili Mkuu wa Serikali.
Mwakilishi ametoa pongezi kwa maandalizi mazuri ya maonesho hayo.
Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Winfrida Beatrice Korosso,ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria, (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Naibu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama(Ajira na Uteuzi), Bi. Enziel Mtei.
Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Winfrida Beatrice Korosso,ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria,(kushoto mwenye koti jekundi) akipata maelezo kutoka banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).
Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Winfrida Beatrice Korosso,ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria,(kushoto mwenye koti jekundi) akipata maelezo kutoka banda la Capital Market.
Mwakilishi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Bw.Ipiana Murilo(katikati), ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa Divisheni ya Utaratibu na Huduma za Ushauri wa Kisheria, akipata maelezo akipata maelezo kutoka kwa Afisa Elimu kwa Jamii wa banda la Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevyia, Bi.Anna Tengia kuhusu dawa za binadamu zinazoleta uraibu kwenye banda la Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevyia .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni