Na Daniel Sichula Mahakama, Mbeya
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Joachim Charles Tiganga jana tarehe 24 Januari,
2025, akiwa katika Kituo cha Radio cha Rock FM jijini Mbeya aliwakaribishisha wadau
washeria pamoja na wananchi wa jiji la Mbeya pamoja na viunga vyake katika
uzinduzi wa wiki ya sheria Jumamosi ya tarehe 25 Januari, 2025 katika viwanja
vya stand ya Mabasi Kabwe na siku ya kilele itakayofanyika siku ya tarehe 3 Februari
2025 katika viwanja vya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya.
Katika
Maadhimisho ya mwaka 2025 yenye Kauli Mbiu isemayo, “Tanzania ya 2025: Nafasi ya
taasisi zinazosimamia haki katika katika kufikia malengo makuu ya dira ya taifa
ya maendeleo.” katika uzinduzi wa wiki ya sheria jijini Mbeya utakaoambatana
na matembezi ya kilometa nne kutoka viwanja vya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda
ya Mbeya hadi stendi ya mabasi Kabwe ambapo shughuli nzima ya uzinduzi
itafanyika itaongonzwa na Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Juma
Homera alisema Jaji Mfawidhi.
Mhe.
Tiganga aliwataka wananchi kuwa tayari kwani elimu ya sheria itatolewa maeneo
mbalimbali katika jiji la Mbeya ikiwepo Stendi ya mabasi Kabwe, Stendi ya
mabasi Mbalizi, Stendi ya Uyole na katika Taasisi mbalimbali za Serikali na
ambazo sio za kiserikali.
Akiwa
ameambatana na Hakimu Mkazi Mkuu Mhe. Paul Ntumo pamoja Hakimu Mkazi Mfawidhi
wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Tedy Raphael Mlimba, Mhe. Tiganga alisema
“Tunapowakaribisha wadau mbalimbali wa sheria, wananchi wasifikilie ni polisi,
magereza, waendesha mashataka au mawakili peke yao hata nyinyi wananchi wa
kawaida ni wadau kwani ndiyo mnaoeleta kesi mahakamani na tunawahudumia.”
Aidha,
Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya imeendelea na maandalizi kabambe kuelekea wiki ya
sheria hadi siku ya kilele cha wiki ya sheria kwa kuendelea kuujulisha umma wa
wana Mbeya kwa kufanya matangazo kupitia vipindi mbalimbali vya Radio, mabango
pamoja na gari kuzunguka maeneo mbalimbali ya jiji la Mbeya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni