Na INNOCENT KANSHA-Mahakama, Dodoma
Mahakama
ya Tanzania imepongezwa na wananchi waliotembelewa mtaani na kupewa elimu ya masuala
ya kisheria na kuiomba Mahakama isiishie kutoa elimu katika wiki ya sheria
pekee bali ifanye hivyo mara kwa mara hasa maeneo ya vijijini.
Akitoa
maoni juu za zoezi la utoaji elimu ya kisheria mtaani Mkazi wa Nkuhungu jijini
Dodoma Bw. Juma Issa amesema, Mahakama imepiga hatua kubwa katika kuhudumia
wananchi kwani zamani hatukuzoea kuiona Mahakama ikijishughulisha katika mambo
hayo ya kutoa elimu mtaani ili ni jambo la kupongeza linapaswa kuigwa na
Taasisi zingine za kiserikali.
“Nawapongeza
Mahakama na Wadau wake kwa kutoa elimu nzuri kama hii tuliyoipata hapa leo
kwani, wengine walikuwa hawafahamu wala walikuwa hawajui lakini leo kupitia
gari la matangazo na elimu likiwa na wanasheria wakuu tumejifunza mambo mengi
sana na kufahamu mambo mengi sana tuliyokuwa hatuyajui kwa hiyo tunashukuru
sana muendelee kutembelea Mkoa wa Dodoma kuwasaidia wale ambao hawajui wapate
fursa ya kujua taratibu mbalimbali za uendeshaji wa shughuli za kisheria
waendelee kujua na kuzitambua taratibu hizi asanteni sana,” amesikika akisema
Bw. Issa.
Naye,
Mkazi wa Nkuhungu jijini Dodoma, Bi. Sada Salum Yoram amesema, “nimejisikia
furaha sana kuona Mahakama imeleta watu wa kutupata elimu ya sheria kupitia
wataalum hawa, kwani kuna wakati unaweza kuwa na haki ukakosa haki na kuna wakati
unaweza kuwa huna haki ukapata haki. Mambo ya aina hii ndiyo Mahakama na wadau
wake wanapaswa kuyazingatia kwa umakini mkubwa ili wenye haki wasipoteze haki
zao…
kuna
uwezekano wazazi wetu wamezaa matumbo mengi na tofauti tofauti unakutana na
sintofahamu nyingi mtoto wa mwisho anapata mali nyingi anakuzidi wewe uliyemtanguliwa
kuzaliwa. Kitu kingine hata kama mzazi akiwa muwazi akisha toweka duniani
lazima ndugu wa marehemu watoe maamuzi bila kukusikiliza wewe mtoto mkubwa,”
amefafanua Bi. Sada.
“Nimejifunza
kitu kikubwa sana na naishukuru sana Mahakama ya Tanzania kwa sababu kuna mambo
ambayo nilikuwa siyajui kwa mfano; nilikuwa sijui masuala ya ndoa, kwani zamani
nilijua ili mtu aachane na mweza lazima awe amefunga ndoa kisheria ya
kiserikali au ya dini, lakini sheria inaelekeza kuwa kuna ndoa ya dhana ambayo
uhalali wake ni kuishi pamoja kwa kipindi cha miaka miwili hiyo kisheria
inahesabika kama ndoa halali kisheria. Na pia ili ndoa itenguliwe ni lazima
muishi pamoja kwa miaka miwili ili Mahakama iweze kuwatenganisha haya yote
nimeyapata kupitia elimu hii. Hili ni
jambo kubwa bila Mahakama kuleta elimu hii mimi ningekuwa bado nipo gizani nawapongeza
Mahakama ya Tanzania,” ameongeza Bi. Sada.
Akitoa
elimu Soko la Mavunde Changombe na Majengo Stendi ya Nkuhungu jijini Dodoma kwa
wananchi juu ya masuala ya kisheria kuhusu wosia. Hakimu Mkazi Mhe. Sifa Jacob
amesema, Wosia ni maelekezo ambayo mtu anayaacha juu ya namna mali zake alizozichuma
zitakavyosimamiwa pale mauti itakapo mkuta.
Aidha,
Mhe. Jacob amesema, kuna aina kadhaa za wosia kama vile wosia wa mdomo ambapo
mtu anaeleza mali zake zitasimamiwa na nani na zitasimamiwa vipi au
zitagawanywa kwa nani na warithi wa mali hizo ni akina nani. Vilevile kuna
wosia wa maadishi unaotanabaisha mali za muhusika ni zipi na nani atarithi na
zitasimamiwa na nani.
Mhe.
Jacob amesema, wosia wa maadishi ni lazima uwe umeshuhudiwa na watu wasiopungua
wawili na wosia wa mdomo ni lazima uwe umeshuhudiwa na watu wasiopungua wanne lakini
kama wosia wa maadishi umeandikwa na mtu
asiyejua kusoma ni lazima uwe umeshuhudiwa na watu wasipungua wanne ambao
wanajua kusoma na kuandika kwa usahihi.
Vilevile,
mambo mengine ya msingi ya kuzingatia kwenye wosia Mhe. Jacob amesema, ni
kuzingatia vitu gani vinaweza kubatilisha wosia kwani wosia unaadikwa ili kuja
kuwa na manufaa baadae kwa hiyo kuna vitu lazima mwandishi wa wosia azingatie ili
wosia wake uwe na tija. Mosi ni lazima wosia umtaje waandishi wa wosia husika
na huyo mwandishi wa wosia ni lazima awe mtu mzima na mwenye akili timamu awe
na umri wa zaidi ya umri wa miaka 18 lakini pia ni lazima awe na akili timamu,
awe ameandika wosia huo bila kushurutishwa na mtu yoyote.
“Mtoa
wosia lazima ataje kwenye wosia husika mali anazotaka kuzirithisha lakini pia
ni lazima ataje warithi wa mali hizo na mwisho asaini wosia huo, lakini kama
hajawahi kusoma na kuandika ataweka alama ya dole gumba kuonesha kuwa nyaraka
hiyo ni yake na mwisho kabisa wosia ni lazima uwe na tarehe ambayo umeandikwa,”
amesisitiza Hakimu Mkazi huyo.
Aidha,
Mashariti hayo yasipozingatiwa Mhe. Jacob amesema, wosia huo unaweza kuonekana
ni batili mbele ya macho ya kisheria. Lakini jambo lingine la kuzingatia ni
wapi mtu anaweza kutunza wosia. Wosia unaweza kutunzwa katika Ofisi za Vizazi
na Vifo (RITA) na pia RITA wanaweza kumsaidia mwandishi wa wosia kuandika wosia
wenyewe, Ofisi ya Wakili unayemwamini, ndugu unayemwamini au shahidi
aliyeshuhudia huo wosia, unaweza kutunza Benki au hata kanisani unakoabudu kama
inawezekana.
Mhe.
Jacob ameongeza kuwa, kuna faida nyingi za kuandika wosia kwanza kabisa
unamuelekeza mwandishi nani atasimamia mirathi hiyo, nani atasimamia pindi
mauti inakukuta, moja ya jambo ambalo linasumbua sana baada ya mtu kufariki kwenye
utambuzi wa nani mwenye sifa na vigezo vya kusimamia mirathi ni nani asimamie
mali za marehemu.
“Kuna
watu wanafikira potofu wanafikiri akiwa msimamizi wa mirathi atakuwa mmiliki wa
mali hizo au kwa namna yoyote atafaidika na mirathi wanang’ang’ania kusimamia
mirathi. Lakini kingine wosia unamuwezesha mwandishi kutaja mali zake na kubainisha
ni nani atarithi mali hizo, hivyo muhusika anaweza kutaja mali zake na kuondoa
ugomvi wa watu wanaojikweza kuwa warithi halali wa mali za marehemu au ni
watoto wa marehemu au ndugu wa marehemu wa karibu wosia unaondoa huo
mkanganyiko,” ameongeza Mhe. Jacob.
Faida nyingine aliyoisema Mhe. Jacob ya kuandika wosia ni kulinda undugu wa wanafamilia atakao waacha marehemu baada ya kifo chake na kuondoa sintofahamu miongoni mwao na kuepusha tabia zisizofaa kama vile kupora mali za marehemu na hata kutoana uhai, kutiana uchizi bila sababu bila sababu za msingi.
Mahakama kijiwe nongwa cha kawahawa Chang'ombe jijini Dodoma elimu ikitolewa kwa wananchi.
Mama Mjasiliamali soko la Mavunde Mang'ombe jijini Dododma akipitia
kwa makini kipeperushu cha elimu ya masuala ya sheria
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni