Na Magreth Kinabo- Mahakama, Dodoma
Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama leo tarehe 24 Januari wafanya ziara kwenye Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania liliopo jijini Dodoma, kwa ajili ya kutembelea Chumba Maalum (Judiciary Visual Situation Room), ili kuweza kufahamu jinsi kinavyofanya kazi ya kutoa taarifa mbalimbali zinazoendelea katika Mahakama zote nchini.
Makamshina hao ni Tom Nyanduga na Dosca Mutabuzi wakiongozana na Kamshina wa Tume hiyo na Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Dkt. Gerald Ndika walifika katika jengo majira ya saa 4:00 asubuhi na kupokelewa na Mtendaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Bw. Victor Florence Kategere, ambaye aliwapeleka kwenye chumba hicho.
Mara baada ya kuwasili katika Chumba hicho, Makamshina hao walipokelewa na Maafisa wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA),ambao walionesha jinsi kinavyaofanya kazi.
Afisa TEHAMA Mkuu, Bi. Priscilla Joseph, ambaye aliwaoongoza Maafisa wenzake kwa kutoa maelezo kuhusu ufanyaji kazi wa mifumo mbalimbali iliyoko ndani ya Chumba hicho, hususan Mfumo wa Usajili,Uendeshaji na Usimamizi wa Mashauri wa Kielektroniki (e-CMS) ambao umeanza kutumika tangu mwezi Novemba, 2023, Mfumo wa Kituo cha Huduma kwa Mteja(Call Center) na Mfumo wa Huduma za Dawati la Msaada(Help Desk).
Baada ya kupata maelezo hayo Makamishna hao, walionesha kufurahishwa na utendaji kazi wa Chumba hicho na kutoa pongezi kwa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Teknolijia ya Habari na Mawasiliano kutokana na juhudi zake kuanzisha Chumba hicho cha kitaalamukinachohusika kuzalisha,kuchambua,kuchakata,kusimamia na kutoa taarifa mbalimbali za Mahakama.
Picha ya pamoja ya Makamishna hao na Mtendaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Bw. Victor Florence Kategere(wa kwanza kushoto), wakiwemo Maafisa TEHAMA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni