Na Imani Mzumbwe – Mahakama, Songwe
Hakimu
Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Songwe Mhe, Francis Kishenyi jana tarehe 25 Februari,
2025 aliongoza matembezi ya ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki Sheria Mkoa wa Songwe
na kutoa rai kwa wananchi kuitumia wiki hiyo kupata elimu ya masuala mbalimbali
ya kisheria ili jamii ifahamu Mahakama inatoa humama gani kwa jamii.
Akizungumza
katika uziduzi huo Mhe. Kishenyi alisema kuwa wiki ya sheria nchini ni fursa
pekee kwa Mahakama kushirikiana na wadau wake katika kujadili changamoto na
mafanikio katika mfumo wa kisheria lakini pia aliongeza kuwa, wiki ya sheria
kutakuwa na mambo mengi ya kuyafanya kama kutoa elimu kwa wananchi katika
maeneo mbalimbali kama vile Stendi, Sokoni, Mashuleni na Mahakama ya Hakimu
Mkazi Songwe.
Naye,
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa Songwe Bi. Farida Mgomi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya
ya Ileje akiwahutubia wananchi amesisitiza na ktoa rai kwa wananchi wa Wilaya
ya Mbozi na Mkoa wa Songwe kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya wiki ya
sheria nchini. Aidha, ameeleza kuwa hiyo ni fursa pekee ya wananchi hao kupata
nafasi ya kujifunza mambo ya kisheria na taratibu mbalimbali pamoja na kujua
haki zao za msingi hususani haki madai.
Mhe,
Farida ameziomba Taasisi mbalimbali kuisaidia Mahakama katika kutoa elimu na
kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabiri wananchi, Vilevile, Bi. Farida
alisema kuwa Taasisi mbalimbali na Mahakama wanatakiwa kutekeleza majukumu yao
kwa uadilifu na uwajibikaji wa hali ya juu wakizingatia misingi ya Usawa, Utawala
bora na Haki kwa wote.
“Naomba
kutoa rai na kuwaasa wananchi na pia kuwasisitiza kutojichukulia sheria mkononi
badala yake wazitumie Mahakama zetu kwani kujichukulia sheria mkononi ni kosa
kisheria na kunaweza kusababisha Visa, Hila na Mauaji mbalimbali yasiyo kuwa na
sababu kwani jamii iliyostaarabika inafuata taratibu za kisheria,” ameongeza Bi.Farida
Naye,
Mtendaji wa Mahakama Mkoa Songwe Bw. Sosteness Mayoka amewashukuru sana Wadau, Watumishi
na Wananchi mbalimbali kwa kujitokeza katika
ufunguzi wa wiki sheria Mkoa wa Songwe na amewakaribisha kuendelea kujitokeza
katika maeneo mbalimbali yaliyopangwa
kutoa elimu kwa wananchi hao ikiwa ni pamoja na eneo la Mahakama ya Hakimu
Mkazi Songwe.
Katika matembezi hayo wadau na Taasisi mbalimbali zilijitokeza kama vile Ofisi ya Mashtaka Taifa Mkoa wa Songwe, TAKUKURU, Police Mkoa, Uhamiaji Mkoa, Jeshi la Zimamoto, Ofisi ya Ardhi Mkoa, Ustawi wa Jamii, Huduma kwa Jamii, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mawakili wa kujitegemea (TLS). Matembezi hayo yalianzia Mahakama ya Mwanzo Vwawa Mjini kupitia njia ya NMB hadi viwanja vya Stendi ya Malori Vwawa Mjini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni