Alhamisi, 30 Januari 2025

ELIMU YA WOSIA, NDOA YAIBUA MASWALI MBEYA


 Elimu ya Sheria ya Ndoa yawagusa Watumishi 

 

Na DANIEL SICHULA, Mahakama Kuu

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu  ya Tanzania Kanda ya Mbeya, Mhe. Joachim Tiganga amekuongoza timu ya wataalamu wa  sheria kutoka Mahakama za Mkoa wa Mbeya katika Utoaji wa Elimu ya kwenye Wiki ya Sheria inaoendelea mkoani  hapa. 

Timu  hiyo ilitoa elimu  katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Mbeya  mada  za Sheria za Ndoa, Uandikaji wa Wosia na Sheria za Mirathi, ambapo watumishi wengi waliguswa na elimu ya uandikaji wa wosia angali ukiwa hai, ikienda sambamba na kujua aina za wosia, faida na hasara zake pale utakapo kuwa haujatuza vizuri na kuufanya siri ya wosia kuvuja.

Aidha mtoa mada katika elimu ya wosia, ambaye ni Jaji Mfawidhi alielezea vitu vya kuzingatia wakati wa uandishi wa wosia kuwa ni mali unazomiliki kwa wakati huo na hata utazochuma au kuuza kwa wakati mwingine ni muhimu kuboresha wosia, majina ya wanufaika na msimamizi wa mirathi na kueleza sifa za muandika wosia kuwa ni awe ametimiza miaka 18, mwaminifu, awe na akili timamu na asiandike wosia akiwa katika shindikizo la mtu yoyote. 

“Sisi Waafrika kutoa wosia kwa maandishi maeneo mengi wanachukulia kama ni kujitakia kifo (uchuro) na ni jambo ambalo mara nyingi mwanamke anazani uandishi wa wosia ni kwa mwanaume tu na sio kwa mwanamke (mke),”alisema Mhe. Tiganga.

Elimu ya Sheria ya mirathi mtoa mada   alielezea juu ya utaratibu wa ufunguaji wa mashauri ya mirathi kwa kuanzia katika Mahakama za Mwanzo na baadae Mahakama ya Wilaya ambayo inapokea maridhiano toka Mahakama ya Mwanzo, ambapo inapokea shauri la mirathi kwenye kiwango cha Tanzania shilingi 100,000,000.

Mada ya ndoa pia iliwagusa washiriki kwa namna yake baada ya kuambiwa mwanamke au mke ana haki ya kukopa kwa jina la mumewe na kuzua maswali mengi kutoka kwa washiriki, ikapelekea mtoa mada kutoa ufafanuzi zaidi juu ya hiyo haki, kuwa mke atakopa kwa mahitaji muhimu ya familia na kabla ya kukopa ni lazima mume apewe taarifa.

Wakati huohuo, Jaji Mahakama Kuu  ya Tanzania Kanda ya Mbeya, Mhe. Musa Pomo aongoza timu ya watoa elimu ya sheria kutoka Mahakama Kuu ,Mbeya  katika Hospitali ya Halmashauri Mbalizi,  ambapo Mhe. Jaji na timu yake walipokelewa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Martin Mbwile.

Katika mada zilizowasilishwa, washiriki waliguswa sana na Sheria ya Ndoa katika ndoa dhania, ambapo mtoa mada aligusia hasara nyingi zinazotokana ndoa dhania na kuelezea kwamba ndoa dhania ni ndoa ambazo mke na mume wanaishi pamoja kwa muda usiopungua miaka miwili na hasara zake ni kwamba haina talaka na haina usajili ndio maana inapelekea wahusika kukosa haki zao za msingi pale wanapotengana.

Aidha washiriki waliweza kupata elimu juu ya kuwepo ndoa za Kidini,Kimila na Kiserikali ambapo ndoa hizo zinakuwa zimefungwa na kusimamiwa na mtu mwenye uhalali wa kufungisha hizo ndoa. Na wanandoa katika ndoa hizo wanahaki zao ambazo mtoa mada aligusia baadhi ikiwemo, haki ya tendo la ndoa kwa wanandoa na kuheshimiana.

Mwisho uongozi wa BOT Mbeya na Hospitali ya Halmashauri Mbalizi walitoa shukrani zao kwa Mahakama  Kuu Mbeya kwa kuwezesha timu za Majaji, Mahakimu, Mawakili wa  Waserikali na Mawakili wa Kujitegemea, wakiwemo wadau mbalimbali wa washeria kufika katika Taasisi zao kutoa elimu kwa kipindi hichi cha Maadhimisho ya Wiki ya Sheria.

Pia Mkurugenzi wa BOT  Mbeya, Dkt. James Machemba aliomba kuwa watahitaji kupatiwa elimu zaidi kuhusiana sheria za mirathi na ndoa.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya, Mhe. Joachim  Tiganga,akitoa mada  wakati wa utoaji wa elimi ya wosia.

 Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya, Mhe. Joachim  Tigangakatikati) akiwa na  Naibu Msajili  wa Mahakama hiyo, Mhe.  Aziza Temu (kulia)pamoja  na Mtendaji wa Mahakama Kuu  ya Tanzania Kanda ya Mbeya,  Bi. Mavis Miti katika ukumbi wa mikutano wa BOT Mbeya. 

matukio mengine katika picha.





(Habari hii imehaririwa na Magreth Kinabo- Mahakama, Dodoma)

Maoni 1 :

  1. Kwa karibu mwaka mmoja, mume wangu aliniacha mimi na watoto wetu wawili. Aliacha kujali, akaacha kupiga simu, na akaondoka kabisa. Nilikuwa nimevunjika moyo, nimechanganyikiwa, na karibu kupoteza tumaini. Kisha siku moja, rafiki yangu aliniambia kuhusu Dkt. Dawn, mtu wa kiroho aliyepewa kipawa na ulimwengu ili kuwasaidia watu kurejesha upendo na amani.

    Mwanzoni, nilikuwa na shaka, lakini kitu kuhusu maneno yake kilinipa amani. Aliniambia haswa kilichokuwa kibaya na kwamba mtu alikuwa ametupa uchawi mkali kututenganisha. Aliandaa kazi maalum ya kiroho na uchawi wa kuungana tena kwa ajili yangu - na ndani ya siku chache, mume wangu alinipigia simu ghafla, akilia na kuomba msamaha.

    Tangu wakati huo, maisha yangu hayajawahi kuwa sawa. Ndoa yetu sasa ni tamu na yenye furaha zaidi duniani. Tunapendana zaidi kuliko hapo awali, na nyumba yetu imejaa vicheko na baraka.

    Lakini sio hivyo tu - Dkt. Dawn pia alisaidia kuondoa bahati mbaya na nishati hasi iliyozunguka familia yetu. Tangu wakati huo, kila kitu kimekuwa laini: amani nyumbani kwetu, maendeleo ya kifedha, afya njema, na furaha safi.

    Ninashukuru ulimwengu kila siku kwa kuniongoza kwa Dkt. Dawn. Kwa kweli ni mtu mwenye nguvu na mwanga wa kimungu. Ikiwa unapitia hali yoyote - huzuni, bahati mbaya, au kuchanganyikiwa - usikate tamaa. Mfikie na uache ulimwengu ufanye kazi kupitia yeye ili kubadilisha hadithi yako, kama vile alivyobadilisha yangu.

    Wasiliana naye kwenye WhatsApp: +2349046229159

    dawnacuna314@gmail.com

    JibuFuta