Na Daniel Sichula – Mahakama, Mbeya
Kufuatia
uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki Sheria, wakazi wa jiji la Mbeya na viunga vyake
wajitokeza kwa wingi kupata huduma mbalimbali kutoka kwa Taasisi zinazotoa
huduma na elimu ya kisheria katika viwanja vya stendi ya mabasi Kabwe jijini
hapo.
Aidha,
katika Banda la Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya limepokea wananchi wa
rika tofauti tofauti waliokuja kwa lengo la kupata elimu za Mirathi, migogogro
ya ardhi, ndoa na baadhi walitaka kujua shughuli na muundo wa Mahakama na namna
unavyofanya kazi kwa kushirikiana na Taasisi zingine ikiwemo Mabaraza ya Ardhi.
Wakati
huo huo, wananchi walifika katika
mabanda ya wadau wa Sheria na Taasisi za Serikali wakiwemo RITA, Polisi Jamii
na Jeshi la Magereza kupata elimu na kupata huduma za usajili wa uzazi na vifo kutoka
ofisi ya RITA bila kusahau Taasisi zisizo za Serikali kama vile Chama cha
Wanasheria Tanganyika (TLS) pamoja na Chuo Kikuu cha Katoliki Mbeya (CuOM)
Kitivo cha Sheria na kuonyesha kuwa mstari wa mbele kutoa huduma mbalimbali kwa
wananchi walifika katika viwanja vya stendi ya mabasi Kabwe kupata elimu ya
sheria
Aidha,
Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC Taifa) walifika kwenye Banda la Mahakama
Kuu Kanda ya Mbeya kwa ajili ya kutoa fursa ya kujua nini kinafanyika kwenye
maadhimisho hayo ya Wiki ya Sheria na kuwapa fursa wananchi kujua ni kitu gani
watapata wakifaka kwenye viwanja vya stendi ya mabasi kwa ajili ya kupata elimu.
Nao
Maafisa Mahakama kama vile Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe.
Aziza Temu, Hakimu Mkazi Mhe. Ayubu Shellimo na Hakimu Mkazi Mhe. Asha Njovu
wakihojiwa na Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Taifa Mbeya walifafanua kwa
undani nini kinafanyika kwa wiki nzima ya maadhimisho ya wiki sheria hadi siku
ya kilele pamoja na kuendelea kuwakaribisha wananchi kufika kwa ajili ya kupata
elimu ya sheria kutoka Taasisi mbalimbali.
Baadhi ya wananchi walifika walishuruku kwa huduma na elimu mbalimbali zinatolewa “Tunashukuru sana Uongozi wa Mahakama Mbeya kwa mualiko wa Taasisi mbalimbali zilizopo hapa kutoa msaada na elimu ya sheria kwani huduma imetufikia kirahisi kabla tulikua hatujui hata tutawafikia vipi kwa kuwa ofisi zao na hata huduma wanazotoa tulikua hatuzijui,” alisema mmoja wa mkazi wa Mbeya.
Wananchi
wakipata huduma kwenye Banda la Chuo Kikuu cha Katoliki jijini Mbeya
Wananchi
wakipata huduma kwenye Banda la Rita
Wananchi
wakipata huduma katika Banda la Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya
Hakimu Mkazi Mhe. Asha Njovu wakihojiwa na Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Taifa
Hakimu Mkazi Mhe. Ayubu Shellimo akitoa elimu kwa mwandishi wa habari kutoka TBC Taifa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni