Jumatatu, 10 Februari 2025

JAJI KAKOLAKI AKABIDHIWA OFISI MAHAKAMA MTWARA

Na HUBERT MAANGA-Mahakama, Mtwara

Jaji Mfawidhi mpya wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mtwara, Mhe. Edwin Kakolaki amekabidhiwa ofisi na mtangulizi wake, Jaji Rose Ally Ebrahim, ambaye amehamishiwa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Morogoro kuendelea na wadhifa kama huo.

Makabidhiano hayo yaliyofanyika hivi karibuni yalishuhudiwa na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mtwara, Mhe. Said Ramadhani Ding’ohi na Mhe. Martha Mpaze, Naibu Msajili, Mhe. Seraphine Nsana, Mtendaji wa Mahakama Mtwara, Bw. Yusuph Issa Msawanga na Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi, Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara, Mhe. Charles Mzava.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Ebrahim aliwashukuru Viongozi na watumishi kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi chote alichokaa Mtwara na kuwaomba kuendeleza ushirikiano huo kwa Jaji Mfawidhi mpya katika utekelezaji wa majukumu ya kimahakama.

Alisisitiza kuwa msingi wa mafanikio ni ushirikiano, upendo, utendaji kazi kwa weledi, uwazi na masikilizano.

Kwa upande wake, Mhe. Kakolaki alishukuru kwa mapokezi mazuri aliyopata kutoka kwa wenyeji wake na kuahidi kuendeleza mazuri aliyoyakuta. Aliomba ushirikiano na kuwahimiza Viongozi na watumishi kufanya kazi kwa weledi na kutoa haki kwa wakati.

Jaji Rose Ebrahim (kulia) akimkabidhi vitendea kazi vya ofisi ya Jaji Mfawidhi mpya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mtwara, Mhe. Edwin Kakolaki (kushoto).


Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mtwara, Mhe. Edwin Kakolaki (kushoto) akikaribishwa na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mtwara, Mhe. Said Ding’oh i(kulia) mara baada ya kuwasili katika ofisi za Mahakama kwenye hafla ya makabidhiano.


Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mtwara, Mhe. Edwin Kakolaki akiwa kwenye picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mtwara. Wengine Mhe. Rose Ebrahim (wa tatu kushoto) aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Kanda ya Mtwara, Mhe Said R. Ding’ohi (wa tatu kulia) na Mhe. Martha Mpaze (wa pili kulia).


Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mtwara, Mhe. Edwin Kakolaki (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara na watumishi baada ya mapokezi mazuri. Wengine ni Mhe. Rose Ebrahim (wa pili kushoto) aliyehamishiwa Mahakama Kuu Kanda ya Morogoro, Mhe. Saidi Ding’ohi (wa pili kulia) na Mhe. Martha Mpaze (wa kwanza kushoto) pamoja na Naibu Msajili, Mhe. Seraphine Nsana (wa kwanza kulia).

(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dar es Saklaam)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni