Na Arapha Rusheke, Mahakama Dodoma
Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo amekutana na kuongea na washiriki wa mafunzo ya kuepuka kutonesha majeraha kwa waathirika wa ukatili wa kingono (Avoiding re-traumatization of victims and witnesses of sexual and gender-based violance) yanatolewa kwa Mahakimu Wakazi, Waendesha Mashtaka na Maafisa Ustawi wa Jamii.
Akizungumza na washiriki hao wanaoendelea na mafunzo hayo jana tarehe 5 Februari, 2025 ikiwa ni siku ya pili ya mwendelezo wa mafunzo hayo, yanayoendelea katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) jijini Dodoma yakiendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Irish Rule of Law International (IRLI) chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Ireland nchini Tanzania.
“Niwapongeze
sana kwa kuchaguliwa na taasisi zenu ambazo zinashiriki mafunzo haya tunapenda
nyie mpate kile ambacho kimeandaliwa na wawezeshaji wetu, lakini upande mwingine
tunapenda pia wawezeshaji nao ambao wamewakuta umu ndani wakute tumewachagulia
washiriki sahihi, hii programu tunafanya na watu wa Irish Rule of Law International,
tunapofanya mafunzo ambayo yanakuwa na wadau wengi kuna vitu vingi tunavipata
kama ambavyo mnafahamu kesi Mahakamani hatufanyi peke yetu,” amesema Mhe. Dkt.Kihwelo.
Mhe.
Dkt. Kihwelo aliongeza kuwa, mafunzo kwa namna nyingine yanabadilisha watu na kuwafanya
waongeze umakini kama mnavyofahamu haiwezi kuwaleta watu wote kwa wakati mmoja,
hivyo ninyi mliopo hapa mwende mkawape wenzenu ujuzi na maarifa mliyoyapata
kwenye mafunzo haya.
“kuna
kitu kimoja ambacho nilisema nikiseme kwa sababu ndicho tunachokitegemea
mkitoka hapa, mafunzo haya mlioyapata mkayafanyie kazi hilo ndiyo lengo kubwa zaidi, na pia
tunategemea sana kupata matunda mazuri baada ya kutoka katika mafunzo haya. Niwapongeze
kwa fursa hii na niwashukuru sana na kuwatakia kila la kheri, ninawashauri
mkirudi katika vituo vyenu vya kazi jitahidini mlichokipata hapa muwafundishe
na wenzenu,” amesema Mhe. Dkt. Kihwelo.
Mhe.
Dkt. Kihwelo amehitimisha kwa kuwataka washiriki wa mafunzo hayo kufanya kazi
kwa ushirikiano ili kufanya kazi iwe rahisi na yenye ufanisi mkubwa.
.jpg)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni