Alhamisi, 6 Februari 2025

MAHAKAMA KUU MBEYA WATEMBELEA NA KUFANYA MATENDO YA HURUMA GEREZANI

Na. Daniel Sichula-Mahakma Mbeya

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga aliwaongoza Watumishi wa Mahakama hiyo kutembelea Gereza la Ruanda lililopo Jijini Mbeya hivi karibuni kupeleka misaada mablimbali ya kibinadamu katika Gereza hilo.

“Watumishi wa Mahakama na wadau wengine wa sheria tunawajali, tunayo furaha kufika hapa kuwapatia elimu pamoja na misaada mbalimbali ya kibinadamu katika Maadhimisho haya ya wiki na siku ya Sheria Nchini,” alisema Jaji Tiganga.

Vilevile, Mhe. Tiganga alielezea kuwa, tukio hilo la kupeleka misaada kwenye Gereza ni kuonyesha upendo kwa Wafungwa waliopo katika Gereza hilo na kuendelea kwa kusema kuwa watakuwa wakifanya hivyo mara kwa mara kwa wafungwa hao na wa Magereza mengine yaliyopo katika Mkoa huo wa Mbeya.

Naye, Kamishina Msaidizi wa Gereza hilo Bw. Mwitiki Kupya kwa niaba ya Uongozi wa Gereza hilo aliwashukuru Mahakama Kanda ya  Mbeya pamoja na wadau wote wa sheria kwa kujitoa kwao kwa hali na mali kuwasaidia wafungwa pamoja na mahabusu waliopo gerezani hapo.     

“Misaada hii ni ishara tosha kuwa Mahakama ya Tanzania walivyo na upendo kwa Magereza hapa Nchini ni mategemeo yangu mtaendelea kutupa misaada hii kwasababu ina mssada mkubwa kwa wafungwa,” alisema Kamishina Msaidizi. 

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga akisalimiana na Kamishina Msaidizi wa Gereza hilo Bw. Mwitiki Kupya mara baada ya kuwasili Gereza la Mkoa wa Mbeya Ruanda kwa ajili ya kutoa elimu na kufanya matendo ya huruma kwa wafungwa na Mahabusu.


Sehemu ya watumishi wa Mahakama na wadau waliotembelea Gereza hilo wakipata maelezo kutoka kwa Kamishina Msaidizi wa Gereza hilo Bw. Mwitiki Kupya walipofika kufanya matendo ya huruma wa kwanza kushoto ni Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni