Na LUSAKO MWANG’ONDA-Mahakama Iringa.
Katika kuadhimisha Siku ya Sheria nchini, Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Iringa, Mhe. Dustan Beda
Ndunguru amekumbushia ahadi ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa ya kutoa kiwanja
kwa Mahakama ya Tanzania kwa ajili ya kujenga jengo jipya la Makahama Kuu.
Jaji Ndunguru alikumbushia ahadi hiyo jana tarehe 3
Februari, 2025 wakati akiongea na umati wa watu uliohudhuria maadhimisho hayo ambapo
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Peter Serukamba alialikwa kama mgeni maalumu.
“Mhe. Mkuu wa Mkoa, ofisi yako mwaka jana
ilituahidi kutupatia kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Mahakama Kuu
Iringa. Naomba nitumie fursa hii ya uwepo wako hapo kukumbushia utekelezaji wa
ahadi hii, ambayo sisi Mahakama Iringa tunaisubiri kwa hamu sana,” alieleza.
Kuhusu jambo hilo, Mkuu wa Mkoa wa Iringa amesema
ofisi yake italishughulikia na kuhakikisha linatekelezwa mapema kwa kadri
iwezekanavyo.
Katika hatua nyingine, Jaji Ndunguru amewashukuru Wadau
wote wa Mahakama Kanda ya Iringa kwa ushiriano waliounesha tangu ufunguzi wa
Wiki ya Sheria, ambapo wameshiriki kwa mambo mbalimbali, ikiwemo kutoa elimu ya
sheria.
Kadhalika, Wadau hao walishirikiana na Mahakama
katika kufanikisha matendo ya huruma kwa kutembelea na kupeleka mahitaji
mbalimbali katika vituo mbalimbali vya watoto yatima vilivyopo Manispaa ya
Iringa.
Wadau mbalimbali walioshirikikiana na Mahakama
kuanzia kwenye Wiki ya Sheria mpaka kwenye Maadhimisho ya Siku ya Sheria
walitunikiwa vyeti maalumu kama alama ya shukrani na pongezi kwa ushiriki wao.
Maadhimisho ya Siku ya Sheria kimkoa yamefanyika katika Viwanja vya Mahakama Kuu Iringa na kuhudhuriwa na Wadau na Wananchi mbalimbali, huku burudani kadhaa zikianikusha tukio hilo.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya
Iringa, Mhe. Dunstan Ndunguru (aliyesimama juu), ambaye alikuwa mgeni rasmi
kwenye Maadhimisho ya Siku ya Sheria akijiandaa kukagua gwaride maalumu
liliandaliwa na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Peter Serukamba akizungumza katika maadhimisho hayo.
Naibu Msajili
wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, Mhe. Bernazitha Maziku akizungumza jambo
katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini.
Mtendaji wa
Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, Bi. Richard Mkongwa akizungumza jambo katika maadhimisho
ya Siku ya Sheria nchini.
Sehemu ya
umati wa Wananchi wahudhuriaji maadhimisho hayo wakifuatilia hotuba ya Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Iringa Mhe. Dustan Beda Ndunguru
(hayupo pichani).
Kikundi cha Bendi ya Watumishi wa Mahakama Kuu Ka,nda ya Iringa, maarufu kama “Mahakama Band” kikitoa burudani kwa kuimba wimbo maalumu wa madhimisho ya Siku ya Sheria nchini.
(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni