Na IMAN PATSON MZUMBWE – RM, Songwe
Hakimu
Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Songwe Mhe. Francis Kishenyi, amewashukuru
wadau na watumishi wote wa Mahakama Mkoa wa Songwe kwa kushiriki katika zoezi
la utoaji elimu katika maadhimisho ya wiki na siku ya sheria nchini.
Mhe.
Kishenyi ameyasema hayo wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria
Nchini kwa mwaka wa waka 2025 jana tarehe 03 Machi, 2025 katika sherehe
zilizofanyika katika viwanja vya Mahakama ya Mkoa Songwe.
“Nimefurahishwa
na zoezi hili pamoja na muitikio wa wananchi waliojitokeza kupokea elimu,
nawashukuru kwa moyo wa dhati kwani elimu hiyo itasaidia kutatua baadhi ya
migogoro bila kufikishana Mahakamani, nawashauri wadau na wananchi kumaliza
mashauri kwa njia ya usuluhishi kwani kumaliza shauri kwa njia ya usuluhishi
hutumia muda mfupi na kuokoa rasilimali fedha na hii itawafanya wananchi
kufanya shughuli zao za kimaendeleo ili kufanikisha dira ya 2050...
Nawasihi
Mawakili wa Serikali na wa Kujitegemea na wadau wote wa Mnyororo wa haki
kuhakikisha wanajitahidi kuwashauri wadau wetu wakimbilie kwenye usuluhishi
kwani ni njia nzuri inayojenga amani kati ya mtu na mtu, usuluhishi pia ufanywe
na viongozi wa dini na amewaomba viongozi hao katika nafasi zao pale
wanapowapokea wadaawa katika maeneo yao kabla ya kufika mahakamani washauriwe
wamalize kwa njia ya usuluhishi ili kujenga Amani”, alisema Mhe. Kishenyi.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Wilaya Mbozi Mhe. Hamadi Mbega ambaye alimwakilisha Mkuu
wa Mkoa Songwe Mhe. Daniel chongolo ameipongeza Mahakama ya Mkoa wa Songwe kwa
kazi nzuri wanayoifanya na ameeleza kuwa
wataendelea kushirikiana nayo na kuhakikisha inafanya kazi zake bila kuingiliwa, pia amewasihi Mawakili
wa Serikali na Kujitegemea kuwa na jukumu la kuisaidia Mahakama katika zoezi
zima la kufanikisha utoaji haki kwa
wananchi.
Aidha,
Mwenyekiti wa kamati ya Elimu Mkoani Songwe Mhe, Vitalis Change amesema kuwa
zoezi la utoaji elimu limefanikiwa kwa kiwango kikubwa kwa kuwafikia takribani
watu 3,032 huku tukifanikiwa kuzifikia shule za sekondari kumi (10) na shule za
msingi tisa (9) jumla ya shule zote ni kumi na tisa (19) hicho ni kiwango
kikubwa ukilinganisha na maadhmisho ya wiki na siku ya sheria kwa mwaka wa
2024.
Naye,
mwakilishi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Mhe, Moses Mwampashi, ameeleza
kuwa, chama kimejipanga kimkakati ili kuhakikisha kwamba kinatoa mchango wa
kitaaluma kadiri iwezekanavyo na kama inavyohitajika ili kutekeleza tija na
ufanisi katika malengo ya dira ya Taifa ya maendeleo 2050, aliendelea kwa kusema
baadhi ya mambo ambayo yamekusudiwa kuyafanywa ni pamoja na kuboresha mahusinao
na wadau mbalimbali wa haki hususani mahakama na wadau wengine, pia amesema kua
chama kimejipanga kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu maswala ya haki kwa
ujumla.
Naye,
Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Songwe Bw. Sosteness Mayoka amewashukuru,
wadau, wageni waalikwa na watumishi kwa ujumla kwa ushirikiano wao tangu zoezi
lilipofunguliwa na hadi mwisho kilele cha siku ya sheria nchini ambapo
imehitimishwa tarehe 3, Feburuari 2025.
Sherehe
hizo za siku ya kilele zimehitimishwa katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu
Mkazi Songwe huku wadau mbali mbali wa Mahakama wakiwa wamehudhuria tatika maadhimisho
hayo ya kilele cha siku ya sheria nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni