· Wafundishwa juu ya Mfumo wa Kidigitali wa Tathimini na Mapitio ya Utendaji wa Maafisa Mahakama (ELECTRONIC JUDICIAL OFFICERS OPEN PERFORMANCE REVIEW AND APPRAISAL SYSTEM–e-JOPRAS).
· Waaswa kuendana na kasi ya Mahakama ya Tanzania juu ya Matumizi ya Mifumo ya KITEHAMA.
· Wasisitizwa kuishi kauli mbiu
ya Mahakama ya Tanzania ambayo ni Uadilifu, Ueledi na Uwajibikaji.
Na HILARY LORRY – Mahakama, Lindi
Maafisa Mahakama Mkoa wa Lindi
wamepata mafunzo ya matumizi ya Mfumo kidigitali wa tathmini na mapitio ya
utendaji wa maafisa Mahakama mahususi kwa Majaji na Mahakimu (eJOPRAS).
Mafunzo hayo, yamefanyika hivi
karibuni katika ukumbi wa wazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi yakiratibiwa na
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Mhe. Consolata Peter
Singano pamoja na Afisa Tehama wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Bw. Furaha
Khatibu.
Akizungumza wakati wa ufunguzi
wa Mafunzo hayo Mhe. Singano alisema Mahakama ya Tanzania imeona umuhimu wa
kuanzisha mfumo huu kwa lengo la kuhakikisha uwajibikaji, uwazi na maendeleo endelevu ya
taaluma kwa kuweka malengo yanayoweza kupimwa, kufuatiliwa na kupata mrejesho.
Mhe. Singano aliwakumbusha
Mahakimu juu ya hatua kubwa iliyopigwa na Mahakama ya Tanzania katika Matumizi
ya mifumo ya TEHAMA na kuwataka maafisa hao kuendana na kasi hiyo.
Aidha, aliwasisitiza Mahakimu
kuzingatia maadili ya kazi zao ili waweze kutekeleza majukumu yao ya utoaji
haki kwa ufanisi unaotakiwa bila ya kufanya upendeleo wa aina yoyote kwa wateja
wao.
“Nawasihi kila mmoja wetu
afanye kazi yake kwa uamnifu mkubwa bila ya upendeleo kwa upande wowote, huku
tukitambua kuwa kazi hii tunayofanya si kazi yetu bali ni kazi ya Mungu na
tufanye kwa uaminifu tukiongozwa na kauli mbiu ya Mahakama ya Tanzania ya
Uadilifu, Ueledi na Uwajibikaji. Tukiweza kuishi kauli mbiu hiyo ninayo hakika
kwamba wananchi na jamii kwa ujumla itarithishwa na maamuzi yetu na kuzidi
kurejesha imani ya wananchi juu Mahakama Tanzania na jukumu lake mama la utoaji
haki,” alisema Mhe. Singano.
Afisa Tehama Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi
Bw. Furaha Khatibu pamoja na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi
Lindi Mhe.Singano kwa nyakati tofauti tofauti waliwasisitiza Mahakimu
walioshiriki Mafunzo hayo kuzingatia zoezi la uhuishaji wa taarifa katika
mifumo ya kuratibu mashauri (e-CMS) pamoja na mfumo wa kuratibu mashauri
Mahakama za mwanzo (Primary Court App) kwani mifumo hiyo inafanyakazi sambamba
na mfumo wa Tathimini na Mapitio ya Utendaji wa Maafisa wa Mahakama (e-JOPRAS).
Vilevile, Baada ya Mafunzo hayo
Maafisa Mahakama walipata wasaa wakutembelea na kuona maendeleo ya ujenzi wa
Kituo Kidogo Jumuishi Lindi (MINI IJC LINDI) unaoendelea chini ya kampuni ya
RIVZI ENGENIARING COMPANY LIMITED.
Mafunzo yalihudhuriwa na Hakimu
Mkazi Mkuu Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Mhe. Consolata Peter Singano, Hakimu
Mkazi Mwandamizi Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Mhe. Delphina Kimath na Mahakimu
Wakazi wa Wilaya tano (5) zinazopatikana katika Mkoa wa Lindi pamoja na Mahakimu
wa Mahakama zote za Mwanzo na Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Bi. Quip
Godfrey Mbeyela.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Mhe.Consolata Peter Singano (aliyevaa suti ya dark blue) akiwa kwenye picha ya pamoja na MaafisaV Mahakama walioshiriki Mafunzo ya Mfumo wa Tathimini na Mapitio ya Utendaji wa Maafisa wa Mahakama (ELECTRONIC JUDICIAL OFFICERS OPEN PERFORMANCE REVIEW AND APPRAISAL SYSTEM –eJOPRAS).
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama
ya Hakimu Mkazi Lindi Mhe.Consolata
Peter Singano (aliyevaa suti ya dark
blue) akitoa neno la ufunguzi kwa maafisa walioshiriki Mafunzo ya Mfumo wa
Tathimini na Mapitio ya Utendaji wa Maafisa wa Mahakama (ELECTRONIC JUDICIAL
OFFICERS OPEN PERFORMANCE REVIEW AND APPRAISAL SYSTEM –eJOPRAS).
Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu
Mkazi Lindi Bi. Quip Godfrey Mbeyela (aliyesimama) akitoa neno la ukaribisho
kwa Maafisa Mahakama walioshiriki mafunzo hayo.
Washiriki wakifuatilia kwa makini
mada zinazowasilishwa na Afisa Tehama.
Washiriki wakifuatilia kwa makini mada zinazowasilishwa na Afisa Tehama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni