Jumanne, 4 Februari 2025

SUMBAWANGA YAZINDUZI KITABU CHA UTENDAJI KAZI SIKU YA MAADHIMISHO SHERIA NCHINI

Na Fredrick Mahava - Mahakama, Sumbawanga.

Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Dkt. Deo John Nangela ameshiriki maadhimisho ya sherehe ya siku ya sheria nchini Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Sumbawanga na kuzindua ripoti ya utendaji kazi wa mwaka 2024 zoezi ambalo litakuwa endelevu kila mwishoni mwa mwaka la utaratibu wa kutoa ripoti ya utendaji kazi wa Kanda hiyo.

Ripoti hiyo chenye sura sita imeangazia mambo mbalimbali ya kiutendaji katika Kanda hiyo, ikiwemo historia ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Sumbawanga tangu ilipoanzishwa mwaka 2005 kikionyesha picha za Majaji Wafawidhi waliyowahi kuhudumia Kanda hiyo katika vipindi tofauti hadi mwaka 2023.

Aidha, sura nyingine zimezungumzia hali ya Watumishi, Takwimu za Mashauri, Majengo na viwanga vya Mahakama, matumizi ya mifumo ya kielektroniki, vyombo vya moto vya usafiri pamoja na bajeti inayotumika kuendesha shughuli za Mahakama Kanda ya Sumbawanga.

Akifafanu yaliyomo kwenye ripoti hiyo, Mtendaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Sumbawanga Bw. Machumu Elias Essaba alisema, kitabu hicho ni nyenzo itakayopima utendaji wa Mahakama zote za Kanda ya Sumbawanga mwaka 2025 ikilinganishwa na kazi zilizofanyika mwaka 2024.

Mahakama zote za Sumbawanga zimemaliza mwaka 2024 zikiwa na wastani wa kumaliza mashauri kadri yalivyosajiwa kwa asilimia 103%. Aidha wastani wa kumaliza mashauri ya siku nyingi (disposal rate) ilikuwa asilimia 82%. Mtendaji huyo ameongeza kuwa, Kulikuwa na mashauri mawili peke yake yaliyokuwa kwenye mlundikano wa mashauri. Viwango hivyo vitatakiwa kuongezeka na siyo kurudi tena nyuma.

Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Dkt. Nangela akiwaonesha kitabu chenye ripoti ya utendaji kazi wa Kanda ya Sumbawanga Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa Mhe. Nyakia Ally Chirukile pamoja na hadhara iliyokusanyika kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya sheria.


Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Bw. Machumu Essaba akielezea uandishi wa kitabu hicho pamoja na yaliyomo 

Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Dkt. Deo Nangela akikata utepe na kukifungua kitabu chenye ripoti ya Utendaji kazi Kanda ya Sumbawanga.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni