Ijumaa, 28 Februari 2025

TANZIA; MSAIDIZI WA SHERIA WA JAJI MAHAKAMA KUU KITUO CHA USULUHISHI AFARIKI DUNIA

TANZIA


            Marehemu Frank William Mirumbe enzi za uhai wake.

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha mtumishi wake Mhe. Frank William Mirumbe, Hakimu Mkazi Mkuu aliyekuwa akihudumu Mahakama Kuu ya Tanzania Kituo cha Usuhuluhishi kama Msaidizi wa Sheria wa Jaji.

Kwa mujibu wa Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kituo cha Usuluhishi, Bi. Hellen Mkumbwa marehemu Frank alikutwa na umauti tarehe 27 Februari, 2025 asubuhi katika Kituo cha Afya Segerea alipokuwa akipatiwa matibabu.

Bi. Hellen amesema kuwa, taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwa Baba Mzazi wa Marehemu Tabata Segerea Chama. 

"Marehemu ataagwa Siku ya Jumamosi ya tarehe 01 Machi, 2025 katika viwanja vya wazi Hospitali ya Polisi barabara ya Kilwa (Baracks) na mazishi yatafanyika mkoani Mara Musoma Nyabange Siku ya Jumatatu ya tarehe 03 Machi, 2025," amesema Mtendaji huyo.

Marehemu Frank alizaliwa tarehe 13 Juni, 1985 na aliajiriwa na Mahakama ya Tanzania tarehe 27 Juni, 2012 kama Hakimu Mkazi katika Mahakama ya Mwanzo Uvinza Kigoma. Mnamo mwaka 2019 marehemu alihamishiwa Mahakama ya Rufani kuwa Msaidizi wa Sheria wa Jaji na mwaka 2021 marehemu Frank alihamishimiwa  Mahakama Kuu ya Tanzania Kituo cha Usuluhishi  ambapo alikuwa akihudumu kama Msaidizi wa Sheria wa Jaji hadi alipofikwa na umauti.

Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki kuomboleza msiba huu wa kuondokewa na mpendwa wetu.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni