Ijumaa, 28 Machi 2025

BARAZA LA WAFANYAKAZI LA KITUO JUMUISHI CHA MASUALA YA FAMILIA TEMEKE LAKETI

Na NAOMI KITONKA, Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia- Temeke

Ikiwa ni miezi michache kuelekea sikukuu ya wafanyakazi Duniani, Baraza la Wafanyakazi la Mahakama ya Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke limekutana kujadili masuala mbalimbali yanayohusu maslahi ya wafanyakazi pamoja na jinsi yatakavyosaidia uboreshaji wa huduma za Mahakama.

Baraza hilo lilifanyika jana tarehe 27 Machi 2025 katika Ukumbi wa Mkutano na kuongozwa na Mwenyekiti wake ambaye ni Jaji Mfawidhi wa Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke, Mhe. Mwanabaraka Mnyukwa.

Akizungumza katika ufunguzi wa Kikao cha Baraza hilo, Mhe. Mnyukwa alisema, “tunawashukuru kila mjumbe aliyepata nafasi na kuonesha utayari wa kuwepo mahali hapa ili kujadili mambo muhimu kwa ajili ya mustakabali wa Taifa letu hasa katika Mhimili huu wa Mahakama, sisi kama wawakilishi wa wafanyakazi tunao wajibu wa kuhakikisha wafanyakazi wanafurahia mazingira ya kazi kwa kupewa haki zao na maslahi yao pia kuboreshwa.”

Jaji Mnyukwa alisisitiza juu ya umuhimu wa vikao vya Mabaraza ya Wafanyakazi kwakuwa vinasaidia kuboresha mahusiano baina ya wafanyakazi katika majukumu ya utumishi pamoja na waajiri ikiwa ni pamoja na kupata matokeo chanya katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Kikao hicho kilihudhuriwa na wajumbe mbalimbali wa TUGHE kutoka Mahakama Kuu na Taifa, wajumbe walipata nafasi ya kujadili maoni mbalimbali kutoka kwa wafanyakazi na kufanya uchambuzi wa kina na maazimio yaliwekwa kwa ajili ya kuhakikisha hoja muhimu zinapatiwa majibu sahihi na ufumbuzi.

Wajumbe wengine waliohudhuria kikao hicho ni Mtendaji Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia- Temeke, Bw. Samson Mashalla, Naibu Msajili wa Kituo hicho, Mhe. Frank Moshi, Mjumbe wa TUGHE kutoka Taifa, Bi. Grace Magerezi, Mwenyekiti wa TUGHE kutoka Mahakama Kuu, Bi. Alice Haule, Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Steven Wadi.

Wengine ni Katibu wa Baraza la Wafanyakazi IJC Temeke, Bi. Fatma Jumbe, Katibu Msaidizi wa Baraza la Wafanyakazi IJC Temeke, Bw. David Mbago, Mahakimu Wafawidhi wa Mahakama za Mwanzo, Wilaya na Mahakama ya Watoto pamoja na wajumbe wengine kutoka TUGHE.

Jaji Mfawidhi wa Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia-Temeke na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Kituo hicho, Mhe.  Mwanabaraka Mnyukwa (aliyeketi katikati) akiongoza Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Kituo hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Mahakama hiyo jana tarehe 27 Machi, 2025. Aliyeketi kushoto ni Katibu wa Baraza la Wafanyakazi 'IJC' Temeke, Bi. Fatma Jumbe na kulia ni Katibu Msaidizi wa Baraza la Wafanyakazi IJC Temeke, Bw. David Moris Mbago.

Jaji Mfawidhi wa Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia-Temeke na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Kituo hicho, Mhe.  Mwanabaraka Mnyukwa (aliyeketi mbele katikati) akisisitiza jambo katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Mahakama hiyo kilichofanyika jana tarehe 27 Machi, 2025. Wanaonekana ni sehemu ya wajumbe wa kikao hicho.

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Baraza hilo, Mhe. Mwanabaraka Mnyukwa (hayupo katika picha).

Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Steven Wadi (kulia) akichangia mada katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke kilichofanyika katika ukumbi wa Mahakama hiyo jana tarehe 27 Machi, 2025. Kushoto ni Mjumbe wa TUGHE kutoka Taifa, Bi. Grace Magerezi.

Mwenyekiti wa TUGHE kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania, Bi. Alice Haule akisisitiza jambo katika kikao hicho cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika  tarehe 27 Machi, 2025. 

 

Mwenyekiti wa TUGHE kutoka Mahakama Kuu, Bi. Alice Haule (kulia), Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es salaam, Bw. Steven Wadi (katikati) na Mjumbe wa TUGHE kutoka Taifa, Bi. Grace Magerezi wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Katika Jumuishi cha Masuala ya Familia-Temeke, Mhe. Mwanabaraka Mnyukwa (hayupo katika picha).

Sehemu ya Wajumbe wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wakijadili jambo katika kikao hicho.

Mjumbe wa TUGHE kutoka Taifa, Bi. Grace Magerezi akichangia hoja katika Baraza la Wafanyakazi la Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke lililofanyika kituoni hapo jana tarehe 27 Machi, 2025.

Jaji Mfawidhi wa Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke, Mhe. Mwanabaraka Mnyukwa (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa TUGHE katika ngazi mbalimbali waliohudhuria Kikao cha Baraza la Mahakama hiyo jana tarehe 27 Machi, 2025.


 Jaji Mfawidhi wa Kituo Jumuishi Temeke, Mhe. Mwanabaraka Mnyukwa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi waliohudhuria Kikao cha Baraza la Wafanyakazi jana tarehe 27 Machi, 2025 kituoni hapo.

(Habari hii imehaririwa na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma)



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni