Na Mwinga Mpoli – Mahakama, Mbeya
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Charles
Tiganga amewataka watumishi wa Mahakama mkoani Songwe kufanya kazi kwa bidii na
kuepukana na vitendo vya rushwa kwani ni adui mkubwa wa haki.
Ameyasema hayo jana tarehe 13 Machi, 2025 wakati akihitimisha ziara yake ya ukaguzi mkoani Songwe, ambapo Mhe. Tiganga ameweza kutembelea Wilaya zote za Mkoa huo ambazo ni Wilaya ya Mbozi, Momba, Songwe na Ileje pamoja na Mahakama zake Mwanzo. Aidha, katika ziara hiyo alifanikiwa kutembelea miradi ya ujenzi wa Mahakama za Mwanzo Wilaya ya Momba Kituo cha Msangano na Mahakama ya Mwanzo Wilaya ya Songwe Kituo cha Kanga na kujionea namna ujenzi unavyoendelea.
“Ni vyema tukaridhika na kile kidogo tunachopata cha halali kuliko kikubwa ambacho kitatutia dhambini na kunyima haki za watu, nitoe rai yangu kwenu kuepukana na rushwa kwani ni adui mkubwa wa haki na hivyo kukwamisha malengo makuu ya Mahakama,” alisema Jaji Tiganga.
Vilevile, Mhe. Tiganga aliwaasa watumishi wa Mahakama Mkoa wa Songwe kufanya kazi kwa ushirikiano na kutumia vizuri muda wa kazi ili kuepuka kutengeneza maisha magumu. Aliwasisitiza watumishi hao kujiendeleza kitaaluma ili kujipatia maarifa mapya na kuendelea kuwahudumia wananchi kwa ufanisi na weledi.
“Kushirikiana katika kazi ni jambo jema kwani msipofanya hivyo mtapoteza upendo kazini. Tumieni vizuri muda wa kazi na muishi kama familia moja ili kuepuka chuki baina yenu na kazi zenu zitakua nyepesi, hudumieni wananchi kwa weledi, jiendelezeni kujitafutia maarifa mapya ya kazi,” alisisitiza Jaji Tiganga
Katika
ziara hiyo, Mhe. Tiganga aliambatana na Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu,
Kanda ya Mbeya Mhe. Aziza Emily Temu, Mtendaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya
Bi. Mavis Francis Miti, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi
Songwe Mhe. Francis Mwesiga Kishenyi, Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Songwe
Bwa. Sostenes Mayoka, Mahakimu Wakazi Wafawidhi Wilaya za Mkoa wa Songwe pamoja
na Maafisa Utumishi na Tawala wa Wilaya hizo.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga akiwa
kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Momba.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga akiwa
Kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama ya Mwanzo Ndalambo wilayani
Momba.
Mwonekano wa Mradi wa ujenzi wa Mahakama ya mwanzo Msangano wilayani Momba.
Mwonekano wa Mradi wa ujenzi wa Mahakama ya mwanzo Kanga wilayani Songwe
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga akiwa
kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama ya Wilaya Ileje.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga akikagua
ujenzi wa Mahakama ya mwanzo Kanga.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga akiwa
kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama ya Wilaya Songwe.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga akisaini
katika kitabu cha wageni alipofanya ziara Mahakama ya Wilaya Ileje.
(Habari Hii Imehaririwa na Innocent Kansha-Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni