Na MAGRETH KINABO - Mahakama, Mwanza
Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Dkt.Musstapher Mohamed Siyani ametoa ushauri kwamba suala la uandikaji wa wosia lipewa kipaumbele na watu wote kwa sababu ni eneo linalogusa hisia za watu,kwaniAJ hatua hiyo itasaidia kuepusha migogoro inayojitokeza katika usikilizaji wa mashauri ya mirathi nchini, ikiwa ni hatua ya kuiwezesha Mahakama kutoa haki kwa haraka.
Aidha Jaji Kiongozi amesema kuwa suala uandikaji wa wosia linahusisha pande zote za jinsia yaani na wanaume wanawake, linagusa haki za watu, hivyo jamii ikiwa na utaratibu huo, mashauri ya mirathi yaweza kusikilizwa bila ya kuwepo kwa migogoro.
“Hivyo wakati tunahudumia wengine sisi pia ni wateja tukumbuke tuliangalie jambo hili, amesema Mhe. Jaji Kiongozi.
Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 19 Machi, 2025 na Dkt. Siyani, wakati akizungumza katika Kikao siku tatu cha Mwaka cha Majaji Wafawidhi kilichomalizika leo kwenye hoteli ya Malaika Beach, jijini Mwanza mara baada ya Jaji Mfawidhi wa Kituo cha Utoaji Haki cha Familia (IJC), Temeke Mhe. Mwanabaraka Mnyukwa kutoa uzoefu kuhusu usikilizaji wa mashauri ya mirathi.
Ambaye amesema kuna changamoto kama vile mgawanyo wa mali, cheti cha kifo kugombaniwa, msimamizi wa mirathi kujimilikisha mali za marehemu ambazo zinajitokeza wakati wa usikilizaji wa masahuri ya mirathi na kuwaasa Majaji hao kuhakikisha kuwa warithi wanashirikishwa kwa kila hatua kwenye usikilizaji wa shauri hilo.
Kwa upande wake, Mlezi wa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Jaji Imani Daudi Aboud, akichangia hoja hiyo amesema suala hilo ni jambo la msingi kwa wanawake pia kuandika wosia kwa kuwa hivi sasa wanamiliki vitu vingi, hivyo wawe na mwamkoa wa kuandika wosia mapema.
“Ni vizuri kwa upande wa wanaume wenye wake wawili au watoto wa nje ya ndoa kuandika wosia ambao utarahisisha kugawa mali kwa kila mtu, tuhakikishe hili tunalisimamia,” amesisitiza Jaji Aboud, ambaye alitoa uzoefu wake kupitia Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tanga alipokuwa akihudumu.
Jaji Aboud ametoa ushauri kwa ni vizuri kila Jaji apitie kufanya kazi katika Kituo hicho, maalum kwa masuala ya familia ili kupata uzoefu, kwa sababu bado Majaji wengi wana muda wa kufanya kazi kwa muda mrefu.
Akichangia jambo hilo, Jaji Mfawidhi wa Majakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Kigoma, Mhe. Augustine Rwizile amesema suala la uandikaji wosia katika jamii ni jambo gumu, “hivyo ni muhimu kuliangalia kwa uzito ili familia zetu zisipate tabu tutakapokuwa tumeondoka duniani,”.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt.Mustapher Mohamed Siyani akizungumza jambo wakati wa uchangiaji wa mada ya uzoefu wa usikilizaji wa mashauri ya mirathi leo tarehe 19 Machi, 2025 kwenye Kikao hicho. Kushoto ni Mlezi wa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Jaji Imani Daudi Aboud.
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya (kulia) akifuatilia mada hiyo,wakiwemo Majaji wengine.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni