Na Hilari Herman - Mahakama, Lindi
Watumishi
wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi hivi karibuni walijumuika pamoja na Maafisa
Mahakama na Maafisa wa Kada mbalimbali kupata iftar ya pamoja ikiwa ni sehemu
ya kukutana, kufurahi pamoja na kubadilishana mawazo ili kudumisha ushirikiano
baina yao.
Katika
hafla hiyo iliyowakutanisha watumishi wa kada mbalimbali wa Mahakama hiyo,
ilihudhuriwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Mhe.
Consolata Singano.
Akitoa
neno wakati wa iftar hiyo kwa watumishi wa Mahakama waliofika katika hafla hiyo
Mhe. Singano aliwasihi watumishi hao kuendelea kujirudisha kwa Mwenyezi Mungu
kwa kufanya matendo yanayompendeza Mwenyezi Mungu hususani katika kipindi hiki
cha mwezi mtukufu wa Ramadhan na Kwaresma.
Akinukuu
maandiko mbalimbali kutoka katika vitabu vitakatifu, Mhe. Singano aliwakumbusha
watumishi hao kuishi kwa kufuata misingi ya Imani zao, kupendana, kujaliana na kufanya
kazi kwa pamoja na kushirikiana ili kuleta tija katika maeneo yao ya kazi.
“Kama tulivyokutana hapa kwenye iftar ya pamoja, basi ushirikiano huu uendelee katika maeneo yetu ya kazi kwa kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa,” alisisitiza Mhe. Singano.
Naye,
Msaidizi wa kumbukumbu Mwandamizi wa Mahakama hiyo Bw. Suleiman Chikumba kwa
niaba ya watumishi wote alitoa shukrani kwa Uongozi wa Mahakama hiyo kwa
kuwakutanisha pamoja watumishi wa ngazi na kada mbalimbali katika “iftar ya
pamoja” na kuuomba Uongozi wa Mahakama hiyo kulifanya tukio hilo kuwa ni
endelevu kwani linaongeza ushirikiano baina ya watumishi.
Iftar
hiyo iliitimishwa kwa dua nzito iliyosomwa na Afisa Ugavi Msaidizi wa Mahakama
ya Hakimu Mkazi Lindi Ustaadh Abeid Omar.
Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Mhe. Consolata Singano
alieketi kwenye kiti akiwa na watumishi Wanawake wa Mahakama ya Lindi mara baada ya kupata
iftar.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Mhe. Consolata Peter Singano akitoa neno baada ya Iftar
Afisa Utumishi Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mazi
Lindi Bw. Stephano Morey (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Hakimu Mkazi
Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Mhe. Consolata Singano mara baada ya
kupata iftar.
Afisa Ugavi Msaidizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi
Lindi Ustaadh Abeid Omar akisoma dua
mara baada ya watumishi kupata iftar.
Msaidizi wa kumbukumbu Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Bw. Suleiman Chikumba akitoa neno la shukrani mara baada ya iftar.
Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Mhe. Consolata Singano
alieketi kwenye kiti akiwa na watumishi wa Mahakama hiyo mara baada ya kupata
iftar.
Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Mhe. Consolata Singano (kulia)
akipata iftar pamoja na watumishi wengine wa Mahakama hiyo.
Afisa
Utumishi Mwandamizi Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Bw. Stephano Morey (kwanza
kushoto) akishiriki iftar na watumishi wa Mahakama hiyo.
(Habari Hii Imehaririwa na Innocent Kansha - Mahakama)







Hakuna maoni:
Chapisha Maoni