Jumanne, 18 Machi 2025

JAJI MFAWIDHI MAHAKAMA KUU KANDA YA GEITA AFANYA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI

Na DOTTO NKAJA- Mahakama,Geita

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Geita, Mhe Kevin David Mhina alifungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Kanda hiyo ya Geita tarehe lililofanyika katika ukumbi wa mahakamani hapo hivi karibuni.

Aidha Jaji Mhina amewapongeza watumishi wote kutokana na  kazi nzuri waliyoifanya kwa mwaka mzima.

Katika kikao hicho mada mbalimbali zilijadiliwa, huku alieleza kuwa baraza hili ni muhimu  kwa sababu  linaendeleza mazingira ya kazi yenye tija.

 “Leo ni siku ya pekee ya kujadili mafanikio tuliyopata na changamoto tunazokutana nazo katika kazi zetu za kila siku,” alisema Jaji Mhina. 

Alitoa rai kwa watumishi hao, kuwa wao ni wawakilishi watumishi wenzao kuwa wawe huru kutoa hoja na zitapokelewa na kufanyiwa kazi.

Mjumbe wa kikao hicho ambaye alikuwa Mwenyekiti wa waliyoifanya Siku ya Wanawake Duniani, Bi. Masalu Cosmas Kisasila ambaye ni Mtendaji wa Mahakama hiyo, aliomba kukadhidi Matendo ya Huruma waliyokuwa wameyapanga kuyafanya Siku hiyo.

Bi. Kisasila alimshukuru Mungu kwa niaba ya wanawake wote Kanda hiyo kwa kufanikisha lengo lao la Matendo ya Huruma na kusema “kwa kuona kuwa nyenzo kubwa za kuyafikia malengo katika kazi zetu za Mahakama ni kuwa wabunifu katika vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA).

“Sisi wanawake Kanda ya Geita tuliamua kuwanunulia VISHIKWAMBI (Tablet) Mahakimu Wafawidhi wa Mahakama za Wilaya, Mahakama ya Hakimu Mkazi, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Geita na Makarani wa Majaji wetu,alisisitiza. Bi. Kisasila.

 Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo ia iwakabidhi walengwa wa vifaa  hivyo.

Baada ya makabidhiano hayo kikao cha Baraza kiliendelea kwa kujadili hoja mbalimbali za watumishi ikiwa ni Pamoja na Bus kwa ajili ya watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Geita ili liwasaidie katika kupunguza gharama za usafiri pindi wanapoenda na kurudi kazini, watumishi mbali na Mahakimu waliomba waangaliwe kwenye suala la posho ili wazidi fanya kazi katika mazingira yasiyo ya changamoto.Watumishi hao, waliomba wangaliwe kwenye suala la fedha ya mavazi.

 Jaji Mhina aliwahimiza wajumbe wa kikao hicho wahakikishe wamefikisha mrejesho kwa watumishi wenzao kwa yote waliojadili. 

Aliwahasa watumishi waendelee kufanya kazi kwa uadilifu, bidii, ushirikiano na kuendelea kuboresha matumizi ya TEHAMA kwa sababu ya mabadiliko ya kiteknolojia yanayoendelea duniani

Picha ya Pamoja kwa watumishi waliopokea Vishikwambi (Tablet) na watumishi wanawake waliofanya matendo ya huruma kuhakikisha TEHAMA inaenda vizuri katika Mahakama  Kuu ya Tanzania Kanda ya Geita.

Jaji Mfawidhi Kuu ya Tanzania Kanda ya GeitaMhe. Kevin David Mhina ,akipokea Matendo ya Huruma kutoka kwa Mtendaji wa Mahakama Kuu  Tanzania Kanda ya Geita,Bi. Masalu Cosmas Kisasila ambaye alikuwa Mwenyekiti katika kusherekea hafla fupi Siku ya Wanawake Duniani.

 Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ChatoMhe. Anamalia Mushi akipokea kishikwambi kutoka kwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu  ya Tanzania Kanda ya Geita, Mhe. Kevin David Mhina(kushoto). 

Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Kanda ya Geita, Mhe. Cleofas Wanae akipokea kishikwambi kutoka kwa  Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu  ya Tanzania Kanda ya Geita, Mhe. Kevin David Mhina. Ambaye amewapongeza   )Wanawake Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Geita kwa kuiona TEHAMA kuwa ni chachu katika utekelezaji wa majukumu kwa ufanisi na haraka.

 

(Habari hii imehaririwa  na MAGRETH  KINABO-Mahakama, Mwanza)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni