Jumanne, 18 Machi 2025

JAJ I MHINA : HAKIKISHENI MNAWAHUDUMIA WATEJA KWA UFANISI


NA DOTTO NKAJA -Mahakama, Geita

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Geita, Mhe. Kevin David Mhina  amewasisitiza watumishi wote Kanda hiyo kuhakikisha kwamba wanawahudumia wadau na wateja wa Mahakama hiyo kwa ufanisi na weledi, wanapotekeleza majukumu yao ya  kila siku. 

Aidha Jaji Mhina amefafanua kwamba suala la maadili sio kwa Mahakimu pekee, kama ilivyokuwa hapo zamani, ambapo maadili yalikuwa yanaangaliwa kwa Mahakimu tu lakini kwa sasa ni kwa watumishi wote wa Mahakama.

Jaji Mhina alizungumza hayo akiwa na Mahakama hiyo,Mhe.Jaji Griffin Mwakapeje Wilayani Nyang’hwale tarehe hivi karibuni, ikiwa ni kikao cha tano kufanyika kupitia   Mwaka  wa Fedha 2024/2025.

“Tuwashughulikia wadau/wateja wa Mahakama hiyo kwa ufanisi na weledi, hivyo ni jambo la muhimu kuendelea kuwahamasisha watumishi wote wajitahidi s katika kuhakikisha wanawahudumia vyema wateja katika Mahakama hiyo.

Viongozi wengine aliozungumza nao ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Geita, Mhe. Fredreck Lukuna, Wahe. Mahakimu Wafawidhi wa Mahakama Hakimu Mkazi na Wilaya, Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Geita, Bi. Masalu Cosmas Kisasila na Maafisa wa kila kitengo katika Kanda   ya Geita.

Jaji Mfawidhi huyo aliwataka watumishi hao, pia kuangalia Mienendo ya Mipango Mikakati(Road Map) ya mambo waliyokuwa wameyazungumuza na kuyapa kipaumbele katika kikao kilichopita. Mambo hayo ni uaminifu katika shughuli Mahakama,kuepuka vitendo vya rushwa na ubadhilifu kazini, uvivu na kutofika kazini bila sababu.

Wajumbe wa kikao hicho na watumishi wote kwa kuendelea na matumizi ya  Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ingawa kuna changamoto ndogondogo lakini wajitahidi kutekeleza majukumu yao kwa wakati.

Aliwaahasa Naibu Msajili na Mtendaji wa Kanda ya Geita, kuendelea kusimamia majukumu yao ili waendelee kuenenda na Dhima ya Mahakama hiyo inavyosema.

Vile vile Maafisa TEHAMA waendelee kufanya ukaguzi na uboreshaji wa vifaa mara kwa mara ili kuondoa kchangamoto ndogongodo zinazojitokeza, ikiwa ni hatua ya kuhakikisha kazi zinaendelea kwa ufanisi zaidi.

 Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Geita, Mhe. Kevin David Mhina (katikati)(kushoto) ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Geita, Mhe. Griffin Mwakapeje na(kulia ni Mtendaji wa Mahakama Kuu  ya Tanzania Kanda ya Geita, Bi.Masalu Cosmas Kisasila wakiwa  meza kuu kwenye   kikao cha menejimenti cha Mahakama Kuu Kanda ya Geita kilichofanyika wilayani Nyang’hwale. hivi karibuni.

 Picha ya pamoja baada ya kikao cha Menejimenti wilayani Nyang’hwale mstari wa mbele (katikati)  ni Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu  ya Tanzania Kanda ya Geita, Mhe. Kevin David Mhina ,(wa pili kushoto) ni Jaji wa  Mahakama  Kuu ya Tanzania Kanda ya Geita,Mhe.  Griffin Mwakapeje (wa pili kulia) ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Geita, Mhe .Fredrick Lukuna, (wa kwanza kushoto) ni Mtendaji wa Mahakama  Kuu ya Tanzania  Kanda ya Geita, Bi.Masalu Cosmas Kisasila na (wa kwanza kulia) ni Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Nyang’hwale, Mhe. Idran Chuvaka.

 Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Geita Mhe. Fredrick Lukuna, akitoa taarifa fupi ya mashauri katika Kanda yake na kutoa mwongozo wa namna ya kumaliza mashauri mapema katika kikao cha menejimenti.


(Habari hii imehaririwa na MAGRETH KINABO-Mahakama, Mwanza)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni