Jumanne, 18 Machi 2025

JAJI MKUU AMEAGIZA JDU KUHIFADHI KUMBUKUMBU ZA MRADI WA MABORESHO

Na MAGRETH KINABO- Mahakama, Mwanza

 

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma 2025 amekishauri Kitengo cha Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania (JDU kuhakikisha kinakasanya nyaraka muhimu  za Mradi wa Maboresho wa Huduma za Mahakama  ili  kuweka historia. 


Akizungumza mara baada ya Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mkuu Kitengo hicho, Mhe.Dkt. Angelo Rumisha kuwasilisha mada juu  ya mradi huo kwenye Kikao cha Mwaka cha Majaji Wafawidhi kinachoendelea katika hoteli ya Malaika Beach, jijini Mwanza leo tarehe 18 Machi, 2025.

 

Mhe. Jaji Mkuu amekiagiza Kitengo cha Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania (JDU) kuhakikisha kinakasanya nyaraka muhimu  za Mradi wa Maboresha wa Huduma za Mahakama  ili  kuweka historia kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo.


Mkuu huyo wa Mhimili wa Mahakama  amesema hayo akiwa anahudhuria,Kikao  hicho, kilicho washirikisha Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda na Divisheni, ikiwa ni siku ya pili, kwa ajili ya kubadilishana uzoefu, ikiwemo kujifunza mambo mbalimbali kutoka Majaji Wafawidhi hao.

 

“Katika kipindi cha muda wa miaka 10 ya utekelezaji ya mradi huu kuna mafaniko yamepatikana.Niliwahi kutembelea Makao Makuu ya JDU kuna makabati makubwa,ambayo ninaamini yamesheheni nyaraka na taarifa …

 

“Zinazohusu mradi huu,hivyo ni vyema zikakusanywa na kuhifadhiwa kwa ajili kuweka kumbukumbu ili historia na kumbukumbu muhimu zisipotee,kwani Chuo Kikuu cha Ardhi kilifanya utafiti  juu ya mradi huu.”  Prof. Juma ameongeza.

 

Hali kadhalika. Jaji Mkuu huyo alimwagiza Mkuu wa Kitengo hicho, kutengeneza mradi mdogo wa muda wa mwaka moja utakaohusu namna gani ya kuzihifadhi   nyaraka na taarifa hizo. Huku akisema wajipe muda mwaka moja kuandika historia hiyo kabla ya  mradi kukamilika.

 

Sambamba na hilo, Jaji Mkuu, Prof. Juma aliwaasa pia Majaji Wafawidhi hao,kuzisoma nyaraka hizo ili kuweza kuwa na uelewa wa mradi huo katika maeneo mbalimbali nchini.

 

Akitoa mada kuhusu Mradi wa Maboresha wa Huduma za Mahakama, Mkuu wa Kitengo hicho ambaye , Mhe. Dkt. Rumisha amewapongeza Majaji hao kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuhakikisha utoaji haki kwa wakati na kupunguza mlundikano wa mashauri kutoka asilimia 10 mwaka 2021 hadi asilimia nne mwakan 2024. Kiwango cha kasi ya uondoshaji mashauri kutoka asilimia 60 mwaka 2021 hadi asilimia 84 mwaka 2024.

 

Amesema Mradi huo kwa sasa umefikia kiwango cha asilimia 85 kwa mujibu wa takwimu za Desemba, 2024 ili uweze kukamilika ifikapo tarehe 30 Juni, 2025.

 

Dkt. Rumisha ameongeza kwamba mradi huo kwa gharama ya kwanza na ya pili unagharamu dola za Marekani milioni 155, zikiwemo gharama uboreshaji wa miundombinu ya Teknolojia ya Habari ya Mawasiliano (TEHAMA) mfano kuwepo kwa Chumba Maalumu cha Mifumo ya kutolea Taarifa muhimu za Mahakama (Judiciary Situation Room), kilichopo katika jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.

 

Amebainisha uwekezaji wa chumba hicho hauelezeki bali watembelee wenyewe ili kushuhudia kwakuwa kuna vijana wameajiriwa mwaka jana kitaaluma ni  wachambuzi wa mifumo (Sytems Analysis) ambao wanajitoa katika kazi hiyo.

 

Dkt. Rumisha  amefafanua kuwa uwekezaji wa  kutumia “screen”mahajamani umeokoa kiasi cha  shilingi milioni 110.

 

Amesema, ni uwekezaji mkubwa ambao umefanyika na ametoa ushauri kwamba Majaji Wafawidhi hao, kupata muda wa kukitembelea na kujionea mafanikio ambayo Mahakama imepiga hatua kwa upande wa TEHAMA.


Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (kulia) akioneshana jambo na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani(kushoto) kwenye Kikao cha Mwaka cha Majaji Wafawidhi kinachoendelea kwenye hoteli ya Malaika Beach, jijini Mwanza leo tarehe 18 Machi, 2025. Ikiwa ni siku ya pili, ambayo imetumika kwa kubadilisha uzoefu.



Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mkuu wa Kitengo cha Maboresho, Mhe. Dkt, Angelo Rumisha akiwasilisha mada kwenye Kikao hicho. 
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mwanza, Mhe.     Dkt. Ntemi Kilekamajenga akionesha kifaa kinachotumika kurekodi sauti ya Jaji au Hakimu kuwa maandishi katika lugha ya Kiswahili au Kiingereza anapoendesha mashauri mahakamani  ili kumrahisishia kazi ya utoaji haki kwa wananchi  kwa  wakati kwenye mfumo wa e-CMSna TTS, alipokuwa akiwasilisha mada kwenye Kikao hicho. 

‘Sreen’ inayoonesha sauti kurekodiwa na kubadilisha sauti ya Jaji au Hakimu kuwa maandishi ili kuwaraisishia kazi ya utoaji haki kwa wananchi kwa wakati.


 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (kulia) na Jaji  Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani(katikati)akiwemo Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu, Dodoma, Mhe. Imani Daudi Aboud(kushoto) wakiwa ni siku ya pili, ambayo imetumika kwa kubadilisha uzoefu, wakifanya mazoezi ya viungo kwa ajili ya kuepukana na magojwa yasiyokuwa ya kuambukizwa kama magonjwa ya moyo, kansa, kisukari na mengine. kwenye Kikao cha Mwaka cha Majaji Wafawidhi kinachoendelea kwenye hoteli ya Malaika Beach, jijini Mwanza leo tarehe 18 Machi, 2025. 

 

 






 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni