Jumatatu, 24 Machi 2025

MENEJIMENTI MAHAKAMA SONGEA YAFANYA KIKAO CHA ROBO YA TATU YA MWAKA

Na NOEL DAUDI- Mahakama, Songea

Menejiment ya Mahakama, Kanda ya Songea, tarehe 21 Machi, 2025 ilifanya kikao kutathmini utendaji kazi katika kipindi cha robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Kikao hicho kilichofanyika wilayani Songea katika ukumbi wa wazi wa Mahakama Kuu kilifunguliwa na Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Songea, Mhe. Dkt. Emmanuel Kawishe, ambaye alikuwa Mwenyekiti.

Taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Mahakama kwa kipindi cha Januari hadi Machi, 2025 iliwasilishwa na Mtendaji wa Mahakama, Kanda ya Songea, Bw. Allan Mwela ambaye alikuwa ni Katibu katika kikao hicho.

Mtendaji huyo akieleza kwenya taarifa hiyo masuala mbalimbali, ikiwemo utawala bora, uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali, ambapo aligusia nguzo namba moja inayohusu utawala na usimamizi wa uendeshaji wa shughuli za Mahakama.

Vile vile aliwasilisha nguzo namba mbili inayohusu utekelezaji wa maagizo ya wakuu wa Mahakama ikiwemo Jaji Mkuu waTanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamisi Juma.

Afisa Bajeti wa Mahakama Kanda ya Songea, Bi. Paulina Kapinga aliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa bajeti ikiwa na maoteo kwa mwaka wa fedha 2024/2025, kiasi cha 978,475,400/-.

Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Songea, Mhe. Dr. Emmanuel Kawishe akizungumza na wajumbe wa kikao cha menejimenti cha Mahakama Kanda ya Songea.

Mtendaji wa Mahakama Kanda ya Songea, Bw. Allan Mwela akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Mahakama.

Afisa Bajeti Mahakama Kanda ya Songea, Bi. Paulina Kapinga, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji bajeti ya robo ya tatu ya mwaka 2024/2025 ya Mahakama Kanda ya Songea.

Sehemu ya wajumbe wakimfatilia kwa karibu Mwenyekiti ambaye hayupo kwenye picha.

Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni